Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa mwakilishi wa wana Tanga atahakikisha fedha za Tasaf zinawanufaisha walengwa na si wengine kama ilivyo sasa.

Mgombea Ubunge ,Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa kuinadi Ilani ya Ccm na kuomba ridhaa ya Wananchi kuwa Mbunge Amesema “Ndugu zangu wanamsambweni nafahamu kero mojawapo inayowasumbua nyinyi na wana Tanga kwaujumla ni fedha za Tasaf kutowafikia walengwa,na hali hii inasabishwa na baadhi ya watendaji wetu wasio waaminifu,ambao huwapatia fedha watu  wasiostahili kupewa Niwaambie   jambo hili nimeanza kulifanyia kazi tutahakikisha wakazi wa Msambweni na Tanga nzima  wanaostahili  kupata fedha za Tasaf  wanapata”Amesema Ummy Mwalimu.

Aidha Ummy ameahidi pia kutatua changamoto ya Elimu kwakusukuma maboresho ya Miundombinu katika Shule ya Msingi Msambweni na Sekondari yake,Daraja kutoka Chuo cha Zaharau hadi Ofisi ya Kata ,na kusafisha dimbwi la Maji linalozalisha mbu katika Mtaa wa Msambweni C .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...