
Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa
Morogoro, Dkt. Christine Ishengoma akizungumza kwenye mkutano wa
uzinduzi wa kampeni Kata ya Magadua Manispaa ya Morogoro.
Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake
wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM kata ya
Magadu.
Wananchi wa Kata
ya Magadu na viunga vyake wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na
Mgombea wa CCM kata ya Magadu.
Mtia Nia Jimbo la
Morogoro Mjini Bwana Salumu Mkolwe akizungumza kwenye mkutano
huo wa ufunguzi wa Kampeni kata ya Magadu.
Mwwnyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro
Bi. Victoria Saduka akizungumza na wananchi wa Magadu
wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Morogoro Manispaa
bwana Hussein Egobano ambaye ndiye Mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa
ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Magadu akiongea na watu
waliofurika kusikiliza Sera za CCM.
Mgombea Udiwani Kata ya Magadu kwa
TIketi ya CCM bwana Kiduka Juma Issa akijinadi mbele ya wananchi wa
Magadu wakati wa uzinduzi huo wa Kampeni za Udiwani kwenye kata
hiyo.
Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake
wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM kata ya
Magadu.
Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake
wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM Kata ya
Magadu.
Na
Calvin Edward Gwabara, Morogoro.
MGOMBEA Udiwani kata ya Magadu kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM) Kiduka Juma Issa amesema akipewa ridhaa kuwa muwakilishi wa
wananchi wa kata hiyo atahakikisha anaiunganisha jamii hiyo na Chuo Kikuu Cha
Sokoine cha Kilimo SUA ili
kufaidi mambo makubwa
yanayofanywa na watafiti wa Chuo hicho Borani Afrika.
Kiduka aliyasema hayo jana wakati wa
Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani zilizofanyika kwwnye Mtaa wa Kididimo na kuhudhuriwa na
mamia ya wakazi wa kata hiyo ambayo imepata bahati ya kuwa na Chuo Kikuu Cha
Sokoine cha Kilimo ambacho kinatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwenye masuala ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi.
“Kata yetu ina bahati ya
kuzungukwa na wasomi wa SUA nitaunda Tume ya watu 7 ambao watakuwa wananishauri njia na mbinu
njema za namna ya kata yetu kukutumia chuo kikuu hiki ili wana Magadu tuwe wa
kwanza kuvuna na kunufaika na uwepo wa Chuo hiki cha pekeee nchini kwenye kata
yetu” alisema Kiduka.
Akizungumzia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa changamoto ya
maji kwenye kata ya
Magadu Mgombea huyo amesema tayari Serikali ya Magufuli imeshatoka
fedha kwa ajili ya
kujenga miundombinu ya maji ambayo tayari imeshaanza kujengwa
na kwamba kukamilika
kwake kutatua kero ya maji kabisa kwenye kata hiyo.
“ Naomba Mnitume kwenye Baraza la madiwani
la Manispaa ya Morogoro nikawatumikie tuhakikishe za habari yetu ya kata ya Magadu
ina öre she’s na kuanza kutoa huduma za kujifungua kwa wakina mama zetu ambao
wanalazimika kwenda Hospitali
ya Mkoa na hospitali zingine kwa sasa, sitaki uheshimiwa nataka
niwe mtumishi wa kweli”
alisisitiza Kiduka.
Pia ametumia nafasi hiyo
kuomba kura kwa Mbunge, Abdulaziz Mohamed Abood
na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kusema
kuwa Oktoba 28 wachague
mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani kutoka
CCM
wasijeweka mafiga mawili ya mawe na figa
moja la udongo ambalo muda wowote linaweza kuangusha chungu.
Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye ufunguzi
wa kampeni hizo za Udiwani Kata ya Magadu, Hussein Egobano ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana
wa (UVCCM) Wilaya
ya Morogoro Mjini amesema amewataka wakazi wa Kata ya
Magadu wasifanye
majaribio kama ambayo zilifanya kata mbili kwenye Manispaa ya
Morogoro kwa kuchagua
upinzani maana miaka mitano yote hakuna
walichokifanya.
Alisema Kata ya Magadu
wenyeviti wake wa mitaa wote wanatoka CCM na
Diwani ndiye Mwnyekiti
wa Baraza la Maendeleo ya Kata (BMK) hivyo wakichagua diwani
wa upinzani watashindwa
kuleta maendeleo maana wataishia kulumbana mambo ya
siasa wakati wananchi
wanataka maendeleo na hivyo kuwataka wamchague Kiduka mgombea wa CCM awe Diwani wao walete
maendeleo kwa haraka.
“Lakini
pia ndugu zangu wa Magadu naleta salamu nyingi kutoka kwa
Mgombea Ubunge
wetu Abood amefanya mambo makubwa ukitaka kujua yote angalia
kitabu cha kazi
alizofanya katika kipindi cha miaka mitano yeye alikataa kuchukua hela
za gari kujinunulia gari
akaamua kuzinunulia gari la wagongwa (Ambulence) na sasa
sote tunalitumia na
magari mengine yanakuja tumeogopa kuyaleta maana watasema
anatoa rushwa ila
akimaliza kuapishwa tu yatatoka” alisema Egobano.
Aliongeza kuwa “ Tumpe kura za kishindo Rais
Dkt. John Magufuli maana amefanya mambo mengi kwenye Taifa letu na Manispaa
ya Morogoro nyinyi ni mashahidi angalieni Soko kubwa la Kisasa, Stand ya Mabasi ya Msamvu,
Stendi ya Mabasi madogo
ya kisasa na barabara za lami na mambo mengine mengi kwenye maji na
afya, ili kumshukuru na
kumtia moyo tumwagie kura za kishindo tarehe 28
Oktoba.
Awali Mgombea Ubunge viti
Maalumu Dkt. Christine Ishengoma ambaye alikuwepo kwenye uzinduzi huo amewataka wakina mama
waache kudanganywa na wapinzani kuwa watawapatia mikopo na kuchukua vitambulisho vyao vya
Kupigia kura maana itawanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura na mwisho wa
siku Wagombea wa CCM wanaowataka watakosa kura zao.
“ Angalieni kazi kubwa iliyofanywa na Mhe.
John Pombe Magufuli nchi nzima, niwaombe tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuchagua wagombea
wa CCM kwenye Udiwani,
Ubunge na Urais kwa kishindo ili kata ya Magadu ndio iongoze Kitaifa
kwa
kuchagua kwa kura nyingi CCM
na wagombea wake” alisema Ishengoma.
Kwa upande wake akitoa salamu kwa niaba ya
Watia nia wa Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini na Mwenyekiti wa UVCCM Mstaafu, Salumu Mkolwe
alisema Kata ya Magadu
imepata bahati sana ya kuwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na
ni fursa kubwa kiuchumi
hasa kupitia walimu na wanafunzi wanasoma kwenye
Chuo hicho.
“ Kuna miradi mikubwa
inatekelezwa na Rais John Magufuli kwenye chuo chetu cha SUA na miradi hii inaongeza
idadi ya wanafunzi wanao jiunga na chuo hiki hivyo kuongezeka huko kwa wanafunzi jamii
ya Magadu inanufaika kwa kuwapatia huduma mbalimbali za vyakula, malazi na mahitaji mengine na
ukiangalia wazee wetu huko mtaani kila mtu nyumbani kwake kapangisha wanafunzi na
hao wanafunzi wanalipa
kodi Magadu inanufaika” alisisitiza Mkolwe.
Uzinduzi huo wa kampeni kwa kata ya Magadu
umeanza jana kwenye mtaa wa Kididimo na kutakuwa na mikutano mingine sita kwenye kila
mtaa pamoja na kampeni za nyumba kwa nyumba kwa mujibu wa Mratibu wa Kampeni kata
hiyo, Profesa, Mombo
ambaye alikuwa Mgombea Ubunge Viti maalumu Mkoani hapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...