NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
Serikali
Mkoani Morogoro imewataka wananchi mkoani humo kujiepusha na makundi
yoyote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani na kufanya vurugu kwenye
vituo vya kupigia kura siku ya oktoba 28 mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo amesema Mkoa wa
Morogoro umejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama katika vituo vya
kupigia kura.
Hata hivyo
Ole Sanare amewataka wananchi wote waliojiandikisha kupigia kura kwenda
kupiga kura siku ya tarehe 28 oktoba 2020 ili kutimiza takwa la
kikatiba la kuchagua madiwani, wabunge na Rais, ambapo zoezi hilo
hutokea mara moja ndani ya miaka mitano.
Mkoa
wa Morogoro una una jumla ya Majimbo 11,kata 214,huku vituo vya kupigia
kura vikiwa 4,774 na waliojiandikisha katika daftari la kudumu la
kupiga kura ni 1,623,629.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...