WAPINZANI zaidi ya 12 katika kijiji cha Vianzi Kata ya Kisegese  iliyopo Tarafa ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na chama hicho.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,Abdallah Ulega ambae pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, akizungumza na wajasiriamali wa kijiji cha Vianzi  Kata ya Kisegese  ambapo amewaahidi kuwaunga mkuno na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Wanachama hao wapatao 12 wametoka katika vyama viwili vya upinzani ambavyo ni (CHADEMA) na ACT-Wazalendo ambapo wameamua kurejesha kadi za vyama vyao na kupatiwa kadi za CCM wakati wa mikutano ya kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega katika kijiji cha Vianzi. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

 

Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kisegese wakila kiapo mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega ambaye  baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama  katika mkutano wa  kampeni jana Oktoba 14,2020.
(Picha na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...