Mkurugenzi huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, amaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ziada Sellah akizungumza wakati wa kikao kazi na Wauguzi na Wakunga Mkoa wa Dar es salaam na kuwataka wauguzi kuwa na kauli nzuri wakati wa utoaji huduma kwa wagonjwa.




Baadhi ya wauguzi waliohudhuria kikao kazi hicho.


WAUGUZI na Wakunga nchini wametakiwa kuepuka kutoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa  kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili na miiko ya taaluma hiyo.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ziada Sellah wakati wa kikao kazi na Wauguzi na Wakunga Mkoa wa Dar es salaam ambapo amesema kumekuwa na tabia chafu ya baadhi ya Wauguzi na Wakunga kujikuta wanatoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa jambo linaloweza kuharibu taswira ya taaluma hiyo.

Aidha Bi. Ziada ametoa wito kwa Wauguzi kujiendeleza kielimu ili waweze kujiongezea maarifa na utaalamu wa kutoa huduma bora na zenye tija kwa wagonjwa.

Pamoja na hayo amewaasa watumishi wa sekta ya Afya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano huku wakizingatia suala la uwazi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Rashid Mfaume na Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga Mkoa wa Dar es salaam wametoa wito kwa Wauguzi kuheshimiana na kuthaminiana katika mazingira ya kazi.

Mkurugenzi huduma za Uuguzi na Ukunga Kutoka Wizara ya Afya yupo Dar es salaam kwa ziara ya kikazi ya siku mbili katika Hospitali mbalimbali za Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za kiuuguzi na kuzungumza na Wauguzi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...