WAWINDAJI, wafugaji
na wakulima wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamepatiwa elimu ya
kufahamu haki zao na kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.
Mafunzo hayo
yametolewa na waelimishaji jamii kupitia shirika lisilo la kiserikali
la Civil Social Protection Foundation (CSP) kwa ufadhili wa shirika la
haki za binadamu la Legal Services Facility (LSF).
Muelimishaji jamii wa
CSP, Obeid Sarakikya akizungungumza wilayani Simanjiro alisema ili
kukuza ushiriki wa kundi hilo kwenye uchaguzi wanapaswa kufahamu haki
zao.
Sarakikya alisema
wanapaswa kufahamu vituo vya kupigia kura vilivyopo karibu na makazi yao
na kutohama kwenye eneo walipo hadi upigaji kura utakapomalizika.
Amesema wanapaswa
kujua kikamilifu siku na muda wa kupiga kura ili tuunde wapange ratiba
ya shughuli zao mapema kwani huwa wanalisha mifugo mbali na makazi yao.
“Mpiga kura anapiga
kura kwenye kituo cha sheria alichosajiliwa na asiyeweza kupiga kura au
kutojua kusoma au kuandika anaruhusiwa kwenda na msaidizi na haruhusiwi
kumchagua mtendaji wa uchaguzi,” amesema.
Mwanasheria wa CSP,
Eliakim Paul amesema utaratibu wa kupiga kura kwa kutegemea hali ya
mazingira ya kila eneo na kupiga kura kituo alichosajiliwa.
Eliakim amesema mpiga
kura anatakiwa kupiga kura kwa amani, utulivu, uhuru na bila
kulazimishwa na kupata usaidizi pale wamapohitaji.
Amesema matarajio ya
wananchi ni kuona sheria na taratibu zote zinafuatwa kabla, wakati na
baada ya kupiga kura, ulinzi na amani unadumishwa na vyombo vya ulinzi
na usalama.
“Pia matarajio ya
wananchi ni kuona wapiga kura wote wanahudumiwa kwa usawa bila upendeleo
isipokuwa kwa wenye uhitaji maalumu,” amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...