Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa ameshika samaki aina ya Jodari akimuonesha mgeni rasmi, Waziri wa Kilimo mhe. Japheth Hasunga wakati wakitembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maadhimisho ya siku chakula duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Njombe leo Oktoba 16,2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo (16.10.2020) kwenye Kilele cha Maadhimisho ya 8 ya kitaifa ya Siku ya Chakula duniani kilichofanyika kwenye viwanja vya Mji mwema Mkoani Njombe.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea cheti cha pongezi kwa Wizara yake kushiriki Maadhimisho ya 8 ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani kutoka kwa Mgeni rasmi wa Kilele cha Maadhimisho hayo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga leo (16.10.2020) Mkoani Njombe.Meneja wa Shamba la Mifugo la Kitulo Bw. Gerald Mashurano (kushoto) akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi wa Kilele cha Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kutoka kushoto) baada ya Mhe. Hasunga kufika kwenye banda la shamba hilo leo (16.10.2020) Mkoani Njombe. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel .






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...