Wanafunzi wa shule ya Mbagala Annex wakiwa na mabango yanayopinga ukatili kwa mtoto wakike.
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Leah Mbunda kutoka dawati la jinsia na watoto kanda maalum Dar es Salaam  akizungumza wakati wa tamasha hilo.
Mhadhiri DUCE na pia  Mwanasaikolojia ya elimu, Simeon Mgode akizungumzi kuhusu ukatili wa mwilini  upande wa walimu na wazazi wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyoandaliwa na WLAC yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Mbagala Annex  jijini Dar es Salaam.

Afisa ustawi wa jamii kata ya Mbagala Gertrude Nyagabona akizungumzia ukatili kwa watoto, wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mbagala Annex jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa miradi ambayo inahusiana na ulinzi wa wanawake na watoto wa kituo cha msaada wa sheria cha wanaake na watoto WLAC, Consolata Chikoti, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mbagala jijini Dar es Salaam

Na Karama Kenyunko Globu ya jamii

WADAU wa maendeleo ya kijamii kutoka Serikalini na kwenye sekta binafsi wameomba kuendelea kujitokeza na kufanya jitihada za kila aina katika kutokomeza ukatili wa aina mbali mbali am bK ao wamekuwa wakifanyiwa watoto na kuwafanya kuishi katika mazingira hatarishi.

Mratibu wa Miradi ambayo inahusiana na ulinzi wa wanawake na watoto kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Consolatha Chikoti amesema hayo leo Oktoba 22, 2020 wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike katika viwanja vya shule ya msingi Mbagala Annex jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Theodosia Muhulo, Consolatha amesema, watoto wote hasa watoto wa kike wana haki ya kulindwa ili watimize ndoto zao, kwa sababu kuna baadhi yao wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia  na kuwafanya kushindwa kutimiza ndoto zao kutokana na mazingira yaliyowazunguka.

"Watoto ni kundi ambalo lipo kwenye hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia, kuna takiwa kuwepo na jitihada za haraka kutoka Serikalini na kwa wadau wa maendeleo ya jamii pamoja na asasi za kitaifa kuhakikisha zinahusika moja kwa moja katika ulinzi wa mtoto." Amesema Consolatha

Consolatha ambae ni Mwanasheria na  Mratibu wa Tamasha hilo, amesema mradi huo ambao unatekelezwa katika Wilaya za Ubungo, Temeke na Kinondoni,  wanaimani utasaidia kuimarisha ulinzi wa watoto. 

Naye, Afisa Elimu Msaidizi Kata ya Mbagala,  Mwalimu Jemima Rengima amesema,  ukatili kwa watoto upo na hali siyo nzuri, kwani watoto wamekuwa wakitoka mitaani kwa ajili ya shughuli mbali mbali ikiwamo kupata elimu, hivyo ni vema wazazi wakashirikiana na walimu katikankutoa taarifa ili kutokomeza ukatili. 

Pia amewaasa wazazi na walezi kuwa pindi mtoto anapoenda kuripoti kufanyiwa kitendo cha ukatili basi wajaribu kulifuatilia, kuanzia ngazi ya chini kama alipata tatizo akiwa shuleni basi waliripoti shuleni, na kama ni nyumbani basi kuna ngazi mbalimbali za kuanzia ikiwemo Serikali za Mitaa hadi kufika polisi.

Amesema tangu watoto hao wapewe mafunzo kwa kushirikiana na WLAC kumekuwa na mabadiliko makubwa , kwa sababu watoto sasa wanaljitambua wamepunguza uoga na kupata ujasiri wa kueleza tatizo pindi tu linapompata bila ya kuona aibu.

Kwa upande wake, Getruda Nyagabona, Ofisa  Ustawi wa Jamii, Kata ya Mbagala amesema wao ndiyo wanaohusika katika masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto, katika maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbio isemayo 'sauti yangu kwa kesho yenye sawa, ikiwa na maana kwamba tumsikilize mtoto wa kike kwa sababu, yupo kwenye kundi ambalo ni hatarishi.

Nae, Tekla Elieza mmoja wa wazazi waliohudhuria maadhimisho hayo amesema, mtoto wa  kike anakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo mara nyingi zinasababisha watoto hao kuingia kwenye mazingira hatarishi na vishawishi.

"Mfano binti anasoma umbali mrefu na kutokana na shule kuwa mbali, kwa hiyo unakuta vijana wa bodaboda anamdanganya kwa kushawishi kumpeleka shuleni ama kurudisha nyumbani, na kwa kuwa mtoto anakuwa ameishachoka anakubali kupanda bodaboda na kujikuta anapelekwa mahali pengine na kufanyiwa vitendo vya ukatili." Amesema 

"Msaada unaotolewa na WLAC umetusaidia sana sisi kama wazazi  yametufanyia wepesi wa kuweza kufuatilia watoto wetu, na tukienda kwenye vyombo husika tunasikilizwa, nina washauri wazazi ambao bado hawajajiongeza, wajiongeze ili tuweze kuwalinda watoto wetu wa kike." Amesema

Aidha Tekla ameishukuru WLAC kwa msaada wa mafunzo walliyotoa na wanayoendelea kuyatoa kwa watoto wa kike na hata wazazi, kwa sababu yamekuwa msaada mkubwa kwao.

Kwa upande wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Kanda maalumu Dar es Salaam, Leah Mbunda amesema katika kuhakikisha ulinzi wa watoto unakuwepo, dawati limekuwa likihakikisha linashughulikia kwa haraka matokeo yote yanayoripitiwa kwa kumtafuta mhalifu na kumkamata kisha kumpeleka mahali panapohusika kwa ajili ya kuchukuliwa sheria.

"Dar es Salaam kuna madawati zaidi ya 20 na wahudumu ni askari waliopata mafunzo waliotapakaa katika vituo vya polisi vikubwa ili kuwashughulikia wahanga wa ukatili. Tunashukuru sana WLAC  kwa kutoa elimu imesaidia sana, wananchi wamepata mwamko, wamepata  uelewa wa kutumia madawati yetu," amesema Mrakibu Mbunda.

Ameongeza kuwa, pamoja na  kupokea malalamiko mengi pia wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali, ambapo kesi nyingi zinazoripotiwa hazifiki mwisho mzuri, kwa sababu zikishafika mahakamani wahanga hawaonekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...