Na Mwandishi wetu, Michuzi TV

CHUO cha Furahika Education College kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kimeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Joseph Magufuli katika kuleta maendeleo kwa kutoa mafunzo ya ufundi bure kwa mabinti na vijana waliokatiza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Chuo hicho tawi la Dar es Salaam David Msuya amesema kuwa, kwa sasa nchi inajenga uchumi wa viwanda hivyo wakaona ni vyema wakazalisha wataalamu watakaoendesha viwanda hivyo.

"Juhudi za Serikali ya awamu ya tano zinahitaji kuungwa mkono na sisi kama Furahika tumekuja na programu hizi za mafunzo ya ufundi kwa vijana ambao ndio chachu kwa Taifa." Amesema.

Kuhusiana na mafunzo yanayotolewa chuoni hapo msuya amesema wanatoa kozi za ufundi kushona, elimu ya Kompyuta, mafunzo ya hoteli, upambaji, mitindo na ususi.

Pia kozi nyingine  zinazotolewa chuoni hapo ni pamoja na Muziki, ufundi ujenzi, uchomeleaji, ufundi wa magari, kilimo, ufundi wa mabomba, ujasiriamali na ufugaji.

Kuhusiana na gharama za mafunzo hayo Msuya amesema kuwa, hakuna gharama zozote isipokuwa wazazi kuchangia rasilimali za kujifunzia kwa vijana wao.

Vilevile amesema kuwa kwa wanafunzi wanaohitimu kozi za ufundi kushona watapatiwa Cherehani mara baada ya kuhitimu mafunzo yao na amewataka vijana, wazazi na walezi kutumia nafasi hiyo ili kuweza kujenga taifa imara na wanaweza kupata taarifa zaidi kupitia barua pepe ya chuoeducationmaendeleo@gmail.com au kupitia mawasiliano ya 0713 708282 au 0678 764884.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...