Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

DAKTARI wa Hospitali ya Dental Clinic, Awadhi Juma aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya mashtaka saba likiwemo shtaka la utoaji Mimba, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje na kulipa fidia ya Sh. Milioni tatu baada ya kupatikana na hatia katika kosa moja la kuendesha hospitali bila ya kuwa na leseni. 

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 18,2020 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Luboroga baada ya kukiri kosa hilo kufuatia makubaliano  ya kukiri shtaka aliyoingia na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini  (DPP.)

Hata hivyo, mshtakiwa Juma ameshalipa fidia ya  sh milioni 3 kama alivyoingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP). 

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Luboroga amesema,  amezingatia makubaliano yaliyoingiwa kati ya mshtakiwa na DPP na pia amezingatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza. 

Amesema kutokana na hali hiyo, mahakama inampa mshtakiwa huyo adhabu ya kifungo cha nje kwa kutofanya kosa kipindi cha mwaka mmoja. 

Aidha, mahakama imemwachia huru muuguzi wa hospitali hiyo Kidawa Ramadhani ambaye alikuwa mshitakiwa katika kesi hiyo baada ya DPP kuwasilisha hati ya kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake. 

Mapema, wakili wa serikali Mwandamizi Materus Marundi alimsomea mshitakiwa huyo shitaka moja lililobakia baada ya mengine kufutwa.

Shtaka linalomkabili ni la kuendesha hospitali binafsi bila kusajiliwa ambapo inadaiwa kati ya Mei 2015 hadi Desemba 4 mwaka 2019 eneo la Sina Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, mshitakiwa huyo aliendesha hospitali binafsi iitwayo kwa Dental Clinic bila ya kuwa na leseni. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...