SHIRIKA la Emirates limepanga kuanzisha kituo kikubwa ambacho kitakuwa kitovu cha kusambaza chanjo ya COVID-19.

Shirika hilo limesema litafungua tena kituo chake cha Emirates SkyCentral DWC huko kusini mwa Dubai, ambacho kitatumika kama kitovu cha anga cha uhifadhi wa na usambazaji wa chanjo hiyo.

Idara ya usafirishaji wa shehena ya Emirates pia imeanzisha timu dharura ili kuratibu maombi kutoka kwa washirika wanaohusika katika usambazaji wa chanjo na kurahisisha usafirishaji kwenda kwa mhitaji.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Emirate na ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wake, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, amesema Dubai ni eneo la kimkakati la kusambaza chanjo hiyo duniani kote.

 “Tuna miundombinu na vifaa vya kusafirisha, na eneo la kijiografia ambalo linaweka masoko yanayowakilisha zaidi ya theluthi mbili ya idadi ya watu ulimwenguni ndani ya eneo la kuruka saa 8. Kuanzisha kituo hiki cha anga hiki ni mradi wa msingi unaotumia mtandao wetu,”amesema.

Kituo hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi duniani katika kusambaza chanjo hizo na kitakuwa kikipokea chanjo hizo kwa njia za anga kutoka kwa watengenezaji ulimwenguni kote kisha kuzihifadhi na kuzisambaza katika mataifa mbalimbali.
Amesema, kituo hicho kina ukubwa wa mita za mraba 4,000 na kinakadiriwa kuweza kuhifadhi na kina uwezo wa kuhifadhi kiasi kikubwa cha chanjo hiyo katika kiwango cha joto na mazingira yanayokubalika kimataifa.

Mbali na vyumba vya baridi vya kutunza chanjo hiyo, Emirates SkyCargo pia itatoa eneo la kuongeza thamani ikiwa ni pamoja na kupaki upya chanjo hizo kwaajili ya kuzisambaza.

 Kupitia ndege mbalimbali zilizopangwa kwenye safari na za kukodisha, msafirishaji wa mizigo ataweza kusafirisha chanjo kwenda sokoni.

 Emirates SkyCargo inauzoefu wa miongo kadhaa uliopatikana kutokana na kusafirisha bidhaa za dawa na chanjo.

Pamoja mtandao wake wa usafirishaji unaofikia zaidi ya vituo 130 katika mabara sita, na eneo la kimkakati la kitovu chake cha Dubai, Emirates SkyCargo itaweza kusafirishaji chanjo haraka.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...