Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Argentina, Diego Maradona amelazwa hospitalini nchini Argentina ingawa hali yake sio mbaya sana.
Maradona mwenye umri wa miaka 60, aliripotiwa kupelekwa kliniki ya Ipensa huko La Plata, karibu na mji Buenos Aires akihisiwa huenda ana mamabukizi ya virusi vya corona.
Maradona anaefundisha klabu ya Gimnasia ya Esgrima. Maradona ambaye alishinda Kombe la Dunia na Argentina mnamo 1986 na anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji wa muda wote nchini Argentina akifatiwa na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...