Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Mheshimiwa Stephen Lujwahuka Byabato ameapishwa Novemba 10, 2020 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma, na kuwa Mbunge kamili wa Jimbo la Bukoba Mjini tayari kuwatumikia Wanajimbo na Wapiga Kura wake.

Mara kadhaa wakati wa Kampeini Mbunge huyo aliyepewa jina la Entoronyonyo (kitu kisafi/kisichokuwa na Doa), alisikika akiwaomba wapiga Kura kutengeneza Mnara wa Mawasiliano kati ya Rais Magufuli na Jimbo la Bukoba Mjini, ambapo amekuwa akisema Jimbo la Bukoba Mjini kwa Miaka Mitano iliyopita limekosa Mawasiliano mazuri na Rais Magufuli kwani hapakuwa na mnara mzuri wa Mawasiliano  (Mbunge) hivyo simu zilikuwa hazipiti.

Mhe. Byabato ambaye ameambatana na Familia yake ameapishwa Rasmi na Wabunge wengine Wateule, muda wa Saa 12:33 Jioni wakati ambapo kiapo hicho awali kilitarajiwa kingefanyika Tarehe 11 Novemba 2020.

Kukamilika kwa kiapo hicho ni kiashiria kwamba Sasa Mheshimiwa Byabato Ni Mbunge Rasmi wa Jimbo la Bukoba Mjini akiwa na Ari na morari ya kuwatumikia Wananchi ailowaomba ridhaa ya Kuwawakilisha Bungeni.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...