Na Jane Edward,Michuzi TV Arusha

.Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dkt Jakaya Kikwete  amewataka vijana wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha  wanashiriki kikamilifu katika jumuiya ya Afrika mashariki na kuweza kuzichangamkia fursa zilizopo.

Aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa vijana wa jumuiya ya Afrika mashariki (YouLead)uliofanyika  mkoani Arusha.

Kikwete alisema kuwa, ushirikiano katika Jumuiya ya Afrika mashariki ulianza muda mrefu na  ni jukumu la vijana kuhakikisha  wanashiriki kikamilifu kwani asilimia 80 ya watu walioko katika jumuiya hiyo ni vijana.

Alisema kuwa,vijana wana wajibu mkubwa wa kuchangamkia fursa zilizopo katika jumuiya kwani sauti yao ni muhimu sana katika jumuiya hiyo.

"uwepo wa jumuiya hii ni muhimu Sana kwa nchi zetu hizi kwani zinawaleta pamoja vijana kutoka mataifa mbalimbali na kuweza kujadili fursa mbalimbali zilizopo na kunufaika nazo ,hivyo vijana hawana budi kuchangamkia fursa hizo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla."alisema .

Naye Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya maendeleo na ushirikiano  wa kimataifa  MS TCDC ,Sara Teri alisema kuwa,mkutano huo umewashirikisha vijana kutoka nchi ya Tanzania,Kenya, Uganda,Burundi,Ruanda na South Sudan .

Sara alisema kuwa,kituo hicho kiliweza kukaa na kubuni njia sahihi ya kuweza kuwaleta vijana pamoja katika kujadiliana changamoto na kushirikishana fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ndani ya jumuiya hiyo kupitia program hiyo ambayo ilianza rasmi mwaka 2014 na kuwakutanisha vijana kutoka nchi mbalimbali.

Sara alisema kuwa,wamekuwa wakifanya mkutano huo kila mwaka na kuwashirikisha vijana na kuweza kuangalia wanafanya nini,mafanikio yao katika maswala mbalimbali ya siasa pamoja na biashara.

Naye Mwezeshaji wa mkutano huo,Abdilah Lugome alisema kuwa,zaidi ya vijana  mia mbili wameweza kushiriki mkutano huo lengo kubwa likiwa ni kujadili agenda za vijana kiuchumi,kisiasa na kijamii huku likiwasaidia vijana kutambua fursa zilizopo katika jumuiya hiyo.

Alisema kuwa, huo ni mkutano wa tano kufanyika na kuwashirikisha vijana ambapo umeandaliwa na kituo cha  cha MS TCDC  kwa kushirikiana na jumuiya ya Afrika Mashariki.

"tuna vijana zaidi ya laki moja wanaofuatilia mkutano huu kwani Kuna fursa za msingi ambazo zinapaswa kuchangamkiwa na vijana ,na tumeomba kuanzishwa kwa baraza la vijana la jumuiya ya Afrika Mashariki ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo kupitia uwepo wa baraza hilo kwani vijana wana utayari mkubwa Sana"alisema Lugome.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...