Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania leo imeanza kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akivutiwa na utendaji kazi wa kampuni hiyo kutokana na kujali wateja wake na huduma bora wanazozitoa.

Akizungumza wakati wa wiki ya huduma kwa wateja, Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam,  Kunenge ameeleza kwamba aina ya biashara wanayoifanya Puma Energy Tanzania inahitaji ubunifu na ushindani mkubwa kwa kuwa inafanywa na kampuni nyingi.

Aidha, kampuni hiyo ambayo inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 50 imeonyesha uwezo mkubwa wa kutoa huduma za viwango vya juu kwa kipindi chote iliyokuwepo nchini.

Amesisitiza kuwa "Navutiwa namna mnavyokuwa karibu na wateja, pia nimesikia mmejipanga kuimarisha huduma zenu katika wiki hii ya huduma kwa wateja, mara nyingi wateja wanapenda kuangalia vigezo kama bei, ubora wa bidhaa na taswira yenu ikoje mbele ya jamii.

“Vingine wanavyozingatia wateja ni usalama wa vyombo vyao, aina ya wafanyakazi mlio nao na mara nyingi wanapenda kulinganisha. Kwa kuwa kampuni hii ipo maeneo mengi barani Afrika wanataka kuona huduma aliyoipata nje ya Tanzania ilingane vilevile,” amesema Kunenge.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema maadhimisho ya mwaka huu yanatokana na mafanikio makubwa waliyoyapata Desemba 2019.


“Maadhimisho yatafanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma duniani, kwa Tanzania tutafanya katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Disemba 4, 2020.

“Wiki hii ni muhimu kwetu kwa kuwa inatupa wasaa wa kukutana na wadau wetu katika biashara ya uuzaji mafuta vituoni, ikiwemo wamiliki wa maduka katika vituo vyetu, waendeshaji wa vituo na kwa namna ya kipekee na wateja wetu,” amesema Dhanah.

Ameongeza biashara yoyote ya mafuta wateja ni watu muhimu ndiyo kitovu cha biashara. Ndiyo maana wameamua kutenga wiki hiyo ya huduma kwa wateja ili kukaa nao karibu kusikiliza maoni kutoka kwao.

“Mkakati wetu ni kumuweka mteja katikati ya kila tunachokifanya kama kampuni, mteja ndio mtu pekee na muhimu katika biashara yetu, lengo kuu la maadhimisho haya ni kuhamikisha wateja na wadau wetu wte wanakumbushwa kwamba kampuni yao inawajali na kuwathamini na kwamba tunahitaji mrejesho wao ili tujitathmini na kuboresha huduma katika vituo vyetu,” alisisitiza Dhanah.

Puma Energy Tanzania ni kampuni iliyosajiliwa Tanzania, ambapo inamilikiwa kwa asilimia 50 na Serikali ya Tanzania   na asilimia 50 na Puma Investments Limited, inajihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji wa bishaa za petroli.

Ina uwezo wa kuhifadhi  jumla ya lita za mafuta milioni 94, ina vituo zaidi ya 60 vya mafuta maeneo mbalimbali ya Tanzania a inahudumia viwanja vinane vya ndege.

Pamoja na hayo amesisitiza mkakati wao ni kumuweka mteja katikati ya kila wanalolifanya ,mteja ndio mtu mmoja wa pekee na muhimu katika biashara yao na lengo kuu la kuadhimisha wiki hiyo ya huduma kwa wateja ni kuhakikisha wateja na wadau wao wote wanakumbushwa kwamba kampuni yao inawajali na kuwathamini.

"Tunahitaji mrejesho na maoni yao ili tuweze kujitathimini na kuboresha huduma katika vituo vyetu Katika mwaka 2020 ambapo dunia imepitia changamoto kubwa ya janga la ugonjwa wa Corona, kampuni ya Puma Energy imekuwa ikiendelea kutoa huduma zake kwa ubora na weledi wa hali ya juu huku ikisaidia wateja wake kupata huduma inayoendana na fedha kwa ubunifu na usalama mkubwa.

"Sisi Puma Energy Tanzania tunatambulika kwa ubora wa bidhaa zetu,sifa hii ya ubora haijaja bahati mbaya bali ni matokeo ya jitihada kubwa za watendaji wote wa Puma kuhakikisha ubora wa hali ya juu unazingatiwa kuanzia mafuta wanapoyahifadhi mpaka yanapoingia kwenye chombo cha usafiri cha wateja wetu.Tunajivunia sana uwezo na sifa yetu hii na tutalinda kwa wivu mkubwa kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,"amesisitiza.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akiweka mafuta kwenye moja ya piki piki (boda boda),akiashiria kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma  Energy Tanzania leo ,pili kulia kwa Mkuu wa mkoa ni Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah pamoja na baadhi ya Watumishi huku watumishi  wengine wa Kampuni hiyo wakifurahia kwa pamoja maadhimisho hayo.Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mmoja wa waendesha boda bada akionesha risiti baada ya kuwekewa mafuta kwa bei inafuu kabisa,ikiwa ni sehemu ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma  Energy Tanzania leo,jijini Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akimsikiliza Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma  Energy Tanzania leo jijini Dar,anaeshuhudia kati ni Mkuu wa Rasilimali watu Afrika na Mashariki ya Kati Kampuni ya Mafuta ya Puma,Loveness Hoyange. Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Es Salaam,baada ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma  Energy Tanzania.Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Pichani katikati ni Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah akiwa sambamba na waendesha piki piki (boda boda) ,Wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa pamoja wakifurahia uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo leo jijini Dar Es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...