KIFO 16/11/2001
BIBIANA (NKAMALI) PETER BASI KWEKA
Bibi yangu Mpendwa na somo wangu pia.Leo umetimiza miaka 19 tangu ulipoitwa Mbinguni kwa BABA.Hatuna cha kusema ,tumebaki kukushukuru tuu kwani hata miaka uliyoishi imezidi ile ya upendeleo.
Tunakumbuka sana uzuri wako,Ucheshi,Usafi na ufanyakazi wako bila kusahau jina lako (BIBI WA SHAMBA).Kweli ulikuwa mfano wa kuigwa.Unakumbukwa sana na mimi somo wako JANE,WAJUKUU WOTE WA KWA BASI SARONGA,MTOTO WAKO WA PEKEE ALIYEBAKI DUNIANI SR.DEVOTA KWEKA CDNK,WA KWEKA WOTE WA NARUMU,WA-ULOMI WOTE WA USWAA-MACHAME,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.
MISA YA KUMUOMBEA IMEFANYIKA LEO ASUBUHI KWENYE KANISA LA MKOLANI –MWANZA
RAHA YA MILELE UMPE EEEH BWANA.....................


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...