Bibi wa miaka sabini na sita (76) Kulusumu Kapinga, akipalilia shamba lake la mpunga, lililopo katika bonde la mtopesi katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga iliyopo katika kata ya Litisha Wilayani Songea.Mhandisi Hassan Mndeme akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu faida ambayo wakulima wataipata baada ya mafunzo hayo
Bw. Joseph Miti Mkulima wa zao la Mpunga katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga, akiongea kuhusu faida zinazopatiana kutokana na kilimo hicho, ambapo alisema kilimo cha umwagiliaji kimekuwa ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hao kwani wengi wamepata ajira na kuongeza kipato.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw.Pololeti Mjema akizungumza na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na waandishi wa Habari hawapo katika picha, Ofisini kwake mapema leo, kushoto, ni Mkurugenzi wa Idara ya Matunzo na Mafunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni.Baadhi ya wakulima wakiwa katika mafunzo wakisikiliza mada inayohusu sheria ya Taifa ya Umwagiliaji.
Na Mwandishi Wetu, Songea
Imeelezwa
kuwa mabonde matatu yaliyopo katika Kijiji cha Nakahuga, Peramiho
wilayani Songea yafanyiwe upembuzi yakinifu ili yaweze kutumika katika
kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni hazina ya serikali ya kupanua eneo la
kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta zaidi ya laki sita zinazo mwagiliwa
kwa sasa mpaka kufikia hekta milioni moja na laki mbili ifikapo mwaka
2025.
Hayo yameelezwa mapema leo Mkoani Ruvuma na Mkuu wa
Wilaya ya Songea Bw. Pololeti Mjema wakati alipokuwa akizungumza na
wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya umwagialiaji waliopo mkoani humo
katika ziara ya kuelemisha wakulima katika skimu za kilimo cha
umwagiliaji za Nakahunga wilayani Songea, Hanga Ngadinda wilayani
Madaba, nakimbande na Msanjesi wilayani Nyasa.
Bw. Mjema alisema
kuwa Serikali kupitia wizara yakilimo, ilishatoa fedha kupitia
halmashauri husika ili uendelezaji ufanyike na inajenga miundombinu hii
kwa gharama kubwa sana hivyo mtoe elimu kwa wakulima ili wajue umuhimu
na namna ya kuchangia katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha
umwagiliaji ili kuwe na utunzaji na uboreshaji thabiti wa
miundombinuhiyo.” Alisisitiza.
Aliongeza kwa kuwakumbusha
wataalamu kusisitiza swala zima la utunzaji wa mazingira kwani wananchi
ndo wanufuaika zaidi wa matumizi ya vyanzo vyamaji huku akiwaasa
wataalam hao kuelimisha kuhusu migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza
kutokana na matumizi ya maji na siyo kuangalia katika kutunisha mfuko
peke yake ili wakulima nao waweze kunufaika.
“Naamni mnaorodha ya maeneo yanayofaa zaidi kwa kilimo cha umwagiliaji kuliko kilimo cha kutegemea mvua.” Alisisitiza.
Awali
akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wakulima katika skimu ya Nakahuga
iliyopo Peramiho, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya uendeshaji na matunzo
kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni alisema mafunzo
hayo yatawasiadia wakulima katika kuelewa kuhusu sheria ya Taifa ya
umwagiliaji ya mwaka 2013 na namna ya kuchangia tozo za huduma za
umwagiliaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...