Chifu Richard Luwawo wa Matumbulu jijini Dodoma akikabidhiwa silaha za jadi mbele ya wananchi wake kuashiria kuanza kutekeleza kazi yake wakati wa wa hafla ya kumsimika iliyofanyika Novemba 11, 2020 jijini humo.

Chifu Mkuu Kanda ya Kati Dodoma Henry Mazengo wa pili (kulia) akimkabidhi Chifu Richard Luwawo (kushoto) wa Matumbulu jijini Dodoma fimbo ikiwa ni ishara ya kuongoza kata ya Matumbulu.

Chifu Mkuu Kanda ya Kati Dodoma Henry Mazengo wa pili (kulia) akimpongeza Chifu Richard Luwawo wa Matumbulu (kushoto) jijini Dodoma mara baada ya kusimikwa kuwa Chifu katika hafla ya kumsimika iliyofanyika Novemba 11, 2020 jijini humo.

Baadhi ya Wageni waalikwa akiwa kwnye hafla ya kumsimikwa Chifu Richard Luwawo wa Matumbulu Novemba 11, 2020 jijini Dodoma.

(Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma)

***************************************

Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Bibi Leah Kihimbi ametoa wito kwa machifu nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia kuwa  mila na desturi imara  ambazo ni msingi madhubuti wa kuendeleza jamii wanayoingoza na taifa kwa ujumla.

Bibi Leah ameyasema hayo Novemba 11, 2020 jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi katika hafla ya kusimikwa uchifu kwa Chifu Richard Luwawo wa Kata ya Matumbulu iliyopo jijini humo.

Akiongea na wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Bibi Leah amewasisitiza machifu kutumia dhamana waliyopewa na wananchi kuhakikisha wanatunza, wanalinda na kuendeleza utamaduni wa mtanzania kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alivyosema, “Taifa lisilo na utamaduni ni taifa mfu”, hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuthamini utamaduni wa taifa.

“Tanzania tuna utajiri mkubwa sana, tuna makabila zaidi ya 150, kupitia maafisa utamaduni waliopo katika kila halmashauri nchini ni wajibu wao kusaidia kutambua maeneo ambayo ni ya kihistoria na yanayotumika kwa matambiko, pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kuhifadhi maeneo hayo” alisema Leah.

Naye Chifu Mkuu Kanda ya Kati Dodoma Henry Mazengo wa Pili  wakati akimuapisha Chifu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu ya uongozi, machifu wanafanyakazi kwa kutumia mafiga matatu ambayo ni machifu, dini pamoja na Serikali ambayo yanafanyakazi kwa kushirikiana ikiwa ni pamoja na  kukemea maovu, yanayokinzana na maadili ya kitanzania.

Aidha, Chifu Mazengo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuthamini mchango wa machifu nchini hatua inayowapa ujasiri wa kutekeleza majukumu vema.

“Rais ametuona sisi machifu na kurudisha cheo chetu ambacho tunakiona kama tunu ambayo ilipotea takriban miaka 40 iliyopita, Dkt. John Pombe Magufuli ni mtu mwenye maono ametuona sisi na kuturudisha katika nafasi yetu ya uchifu, tupo nyuma yake katika kutekeleza majukumu yetu na taifa litazidi kusonga mbele.”

Kwa upande wake Chifu Richard Luwawo wa Matumbulu ameahidi kuendeleza, kusimamia mila na desturi za eneo la utawala wake kwa kushirikiana na wananchi hatua itakayosaidia kuhakikisha mazingira yanatunzwa ili kutunza uasili wake ambayo ni chanzo cha mvua za kutosha kwa ajili ya shughuli za kwaletea maendeleo.

Naye Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago alisema kuwa katika kusimamia mila na desturi, wananchi wa kata ya Matumbulu wapo mstari wa mbele kwani wanatambua wajibu wao kukemea mienendo inayohatarisha maadili ya jamii yao kwa mila na desturi za Kigogo ambapo wazee huwakanya vijana hatua inayosaidia kuendeleza utamaduni wao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...