Picha ya Pamoja ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na watu wenye ulemavu Doroth Mwaluko mara maada ya kufUngua Maadhimisho ya wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyoshirikisha watoa huduma wa sekta ya Afya kutoa huduma ya kupima na ushauri wa Magonjwa hayo.*Ulaji na kutofanya mazoezi ndio vinachangia katika Magonjwa yasiyoambukiza.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa magonjwa yasiyoambukiza ni tishio nchini kwakuwa magonjwa hayo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kwa makundi yote.
Serikali imewataka watoa huduma wa afya watumie lugha rafiki katika utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuwawezesha kuelewa na kuona umuhimu wa kupima afya Mara kwa mara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi utoaji wa huduma mbalimbali zinazohusu magonjwa yasiyoambukiza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu na watu wenye Ulemavu Doroth Mwaluko amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zinaonyesha wagonjwa hawajijui kwasababu ya kutoenda kupima afya zao mara kwa mara.
Mwaluko ameelekeza, tafiti hizo zisaidie kuwafikia wananchi ambao ni wahitaji na waone umuhimu wa kupima afya zao,vinginevyo tafiti zitaendelea kufanyika kufanyika na kila siku tutaendelea kuelezwa hizo tafiti.
Mwaluko amesema kuwa matokeo yake na mchango wake wakufanya wananchi wa Tanzania waweze kupima afya zao unakuwa kwa kiwango kidogo hivyo watoa huduma kujitoa katika kutoa elimu ya afya.
Mbali na hilo amesema magonjwa yasiyoambukiza bado hakijajulikana chanzo chake kulingana na tafiti za wahusika,lakini kwa kiwango kikubwa kinatokana na mtindo wa maisha ya watu,nakubainisha hawafanyi mazoezi ,ulaji haufai na kuna matumizi ya vitu mbalimbali kama tumbaku,pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi .
"Nimefarijika kwenye mabanda huduma zinazotolewa, na nimesikia maelezo mazuri ambapo wahusika wa lishe walieleza mambo mengi yanachangia kupata magonjwa ikiwemo ulaji wa chakula "alisema.
Aidha amesema kuwa kama mwananchi wa Tanzania kumekuwa na ujumbe mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu suala la chakula Bora,ambapo kila mmoja akizungumza anavyojua.
Amewaomba wahusika kuelimisha wananchi ipasavyo ili wale vyakula vinavyofaa kwa wakati muafaka,ili kuondokana na dhana ya ulaji sio tatizo.
"Kwahiyo watu lishe muelimishe vizuri kwa lugha nyepesi ili wananchi wajua wanakula nini na kwa wakati gani na kwa mtindo upi "amebainisha.
Ameeleza kuwa mbali na elimu zao lakini pia wajue na upokeaji wa wananchi kwa wanayoyasema na mitazamo mbalimbali kutokana na mazingira yaliyopo ambapo mkiniambia mazoezi nitasema nafanya kazi nyingi ambapo mtasema haitoshi.
"Ni wajibu wao kuelimisha ili kuona umuhimu vinginevyo mtaendelea kusema kila siku magonjwa yanaongezeka Lakini mkienda kwa undani uelewa bado mdogo"alisema
Pia aliwataka wasisahau kuwa nchi ya Tanzania ina vyakula vya aina mbalimbali kwahiyo kutumia vyakula hivyo kwa kuwapa maarifa mazuri ya chakula kizuri ili kuweza kuepukana na na mgonjwa yasiyoambukiza.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...