Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

FURAHA kwa Watanzania. Ni baada ya  taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ya kukataza mashabiki kuingia Uwanjani kwenye mechi zote za kufuzu AFCON sasa Rasmi Tanzania waruhusiwa.

Taarifa ya kuruhusiwa kwa mashabiki imetolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

TFF, wamesema kuwa CAF wameruhusu watazamaji kwenye mchezo huo wa Kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia utakaochezwa Novemba 17, 2020 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

CAF imeelekeza kuwa, watazamaji watakaoingua ni aslimia 50 ya uwezo wa Uwanja.

Kwa sasa, TFF wanawasiliana na serikali ili kukidhi matakwa ya CAF katika mchezo huo.

Mechi ya kwanza dhidi ya Tunisia itachezwa Novemba 3,2020 Jijini Tunis na kwa sasa Timu ya Taifa ya Tanzania ipo kambini nchini Uturuku ikimalizia kambi ya siku 3 kabla ya kwenda kuwavaa wapinzani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...