MHADHIRI Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)ambae ni Mkuu wa taasisi ya Tanzania Community Networks Alliance(tzCNA), Matogoro Jabhera amesema ameamua kuanzisha ushirika wa huduma ya mawasiliano ya gharama nafuu na kusaidia ushirika huo kwenda digitali na mkakati wake ni kuwafikia watu milioni 20 katika kipindi cha miaka mitano.

Ushirika huo ni wa  aina yake kuanzishwa nchini Tanzania ambao ni tofauti na ushirika wa fedha yaani SACCOSS tofauti ushirika wa mazao yaani Agriculture and MarketingaCooperative Society(  AMCOS) ambao umezoeleka.

Akizungumza kuhusu ushirika huo, Jebhera amesema kwamba lengo lake ni kuwafikishia huduma ya Mtandao watu milioni 20 ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Amesisitiza huo ni mwendelezo wa jitihada zake za kutumia teknolojia ya mawimbi ya televisheni yaani "television white space" kwa ajili ya huduma ya mtandao.

Matogoro amesema "Huu ni ushirika maalumu kwa ajili ya vijana na ushirika huu utatoa fursa za ajira kwa vijana wetu na kwa wananchi wote bila kujali viwango vya elimu zao wala fani zao.
 Aliendelea kufafanua zaidi na kwamba kwa wale ambao wanahitaji kumfahamu zaidi huduma za mitandao hiyo ya ushirika wanaweza kutembea kwenye tovuti yao inayotambulika kwa barua pepe www.tzcna.or.tz


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...