Ofisa afya wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jovin Rweyemamu akizungumza kwenye
kikao kazi cha Mamlaka ya Mji huo.

Wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kikao kazi cha Mamlaka hiyo.

Mjumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Joyce Mwasha akizungumza kwenye kikao
cha Mamlaka hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Evence Mbogo akizungumza
kwenye kikao kazi cha Mamlaka hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
Mamlaka hiyo Christopher Chengula na kulia ni Mkuu wa kituo cha polisi
Mirerani, qqASP Christina Mkonongo.
*******************************************
ILI kupambana na
ugonjwa wa kichaa cha mbwa, wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamejipanga kuhakikisha wanawadhibiti
mbwa wote wanaozuruza ovyo kwa kuwapiga risasi.
Ofisa afya wa Mamlaka
ya Mji mdogo wa Mirerani, Jovin Rweyemamu akizungumza kwenye kikao cha
Mamlaka hiyo alisema hivi karibuni watu wanne wameng’atwa na mbwa wenye
kichaa kwenye eneo hilo.
Rweyemamu mbwa
wanaozurura ovyo wenye vichaa waliwangata watu wanne ambao walitibiwa
kwenye zahanati za mitaani kea sh30,000 kwa kila mmoja.
Alisema mbwa hao wanaozurura ovyo wanapaswa kuchukuliwa hatua kwani watasababisha vifo kupitia ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
“Uking’atwa na mbwa
na usipopata matibabu mapema unapoteza maisha yako hivyo suala hilo
lichukuliwe hatua kwa haraka ili madhara yasitokee,” alisema Rweyemamu.
Mwenyekiti wa mtaa wa
Endiamtu, Nalogwa Mkumbo alisema mbwa wote wanaozurura ovyo wanapaswa
kuchukuliwa hatua na siyo mbwa wenye vichaa pekee.
Mkumbo alisema wao
kama viongozi wa wananchi wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha
wanapambana na tatizo hilo ili lisilete madhara.
Mwenyekiti wa mtaa wa Songambele, Daudi Makala alisema Serikali inapaswa kuchukua hatua kwenye jambo hilo.
Makala alisema kila mfugaji wa mbwa ahakikishe mbwa wake anapata chanjo na kufungiwa kwenye banda.
Hata hivyo,
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Adam Kobelo aliwataka
wenyeviti wa mitaa ya Mji huo kusimama upande wa Serikali Ili
kuhakikisha suala hilo linamalizika.
Kobelo alisema wenyewe hao wanasimamia maeneo yao ipasavyo kwa kuhakikisha mbwa waliopo katika sehemu zao wanapatiwa chanjo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...