Na Pamela Mollel, Longido

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Dkt Jumma Mhina amevitaka vyama vya siasa pamoja na wagombea wao walioshiriki katika uchaguzi Mkuu wa Jimbo hilo kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo Steven Lemomo ili aweze kutekeleza mipango ya maendeleo aliyonayo kupitia chama chake na Halmashauri hiyo

Aliyasema hayo juzi wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Longido ambapo alimtangaza Dkt Lemomo kuwa mshindi halali wa jimbo hilo kupitia chama Cha Mapinduzi

Dkt Mhina alisema kuwa vyama vya siasa katika Jimbo hilo kuwa kitu kimoja kwa kuwa uchaguzi umekwisha na Mbunge aliyepita ni wawananchi wote atakaye waletea maendeleo

"Ndugu wananchi baada ya uchaguzi kuna maisha  baada ya uchaguzi sisi ni ndugu,sisi ni marafiki,sisi ni Jamii moja tudumishe Amani tuliyonayo"alisema Dkt Mhina

Aidha alisisitiza suala la Amani kama ambavyo Rais John Pombe Magufuli anawasisitizia  Watanzania wote

Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amesema kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua mtu ambaye atahamasisha au atashiriki kuwa miongoni wataakao anzisha vurugu au maandamano

Mwaisumbe alisema kuwa maandamano hayo  hayapo kisheria hivyo mtu au kikundi atachukuliwa hatua kali na Serikali haitafumbia macho Jambo hilo

Aidha alisema kuwa wanaofanya hivyo nikutaka madaraka yasiyo halali

"Tunazo tetesi kwa baadhi ya viongozi walioshindwa katika uchaguzi wameamua kuitisha maandamano ya kuleta vurugu na kuvunja Amani tuliyonayo"Alisema Mwaisumbe

Vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi Mkuu nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo CCM, Steven Lemomo kura 61,885 , CHADEMA,Lukas Laizer 1,037 ,CUF Kombo Mkadam 65 ,NRA Juma Feruziyson 21

Idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika jimbo hilo 76,814,waliopiga kura 63,465,idadi halisi waliopiga kura 63,008,kura zilizokataliwa 457.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Dkt Jumma Mhina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...