Mwandishi
wa habari wa kujitegemea wa Mkoani Kilimanjaro, Patrick Chambo
amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, kwenda jela
miezi minane kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.
Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Babati Victor Kimario ametoa hukumu hiyo ya kesi ya CC 14/2019 Novemba 24 mjini Babati.
Hakimu
Kimario ametoa hukumu hiyo baada ya waendesha mashtaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru, Martin Makani na Evelyn Onditi
kuiomba Mahakama hiyo kuendelea na hatua ya hukumu baada ya mshtakiwa
kuruka dhamana.
Chambo
aliruka dhamana ya mahakama hiyo baada ya upande wa mashtaka kukamilisha
ushahidi na Mahakama hiyo kutoa uamuzi mdogo kuwa Chambo ana kesi ya
kujibu hivyo badala ya kujitetea akaruka dhamana na kujinyima haki ya
kusikilizwa ila hati ya kumkamatwa ili atumikie kifungo imeshaandaliwa.
Awali,
Chambo alifikishwa Mahakamani hapo na kushtakiwa kosa la kuomba rushwa
ya shilingi 300,000 na kupokea rushwa ya shilingi 100,000.
Amesema
Chambo aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya kiwanda
cha maji Mati Super brands ya Mjini Babati, akidai kuwa wamekwepa kulipa
kodi.
Amesema Chambo
alimueleza Mkurugenzi huyo kuwa endapo wasingempatia kiasi hicho cha
fedha angewaandika kwenye vyombo vya habari kuwa wanakwepa kodi ya
serikali.
Amesema
Mkurugenzi wa kampuni hiyo alifikisha malalamiko hayo TAKUKURU ambao
waliweka mtego na kumkamata Chambo kisha kumfikisha Mahakamani na
kuhukumiwa.
Mkuu wa
TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Joseph Makungu ametoa rai kwa waandishi wa
habari kuwa endapo watabaini ushahidi wa kukwepa kodi watoe taarifa
Mamlaka ya mapato nchini TRA au TAKUKURU.
Makungu
amesema na kukamatwa kwa Chambo walifanya uchunguzi na kubaini ni kweli
kampuni ya Mati Super brands Ltd ilikwepa kodi zaidi ya shilingi
milioni 5.
"Tuliitaka
kampuni ya Mati Super brands Ltd kulipa kodi hiyo iliyokwepa shilingi
milioni 5 na adhabu ya shilingi milioni 50 kwenye mamlaka ya mapato
nchini TRA na wanaendelea kufuatilia mienendo ya ulipaji kodi wa kampuni
hiyo ili mapato halali ya serikali yasihujumiwe.
"Watu
wa Manyara tukumbuke kuwa hakuna haki wala wajibu hivyo kila mmoja ana
haki ya kufanya biashara halali inayomwingizia faida ila ni wajibu alipe
kodi halali kwa maendeleo ya Taifa" amesema.
Amesema
endapo kuna mwananchi anataarifa ya kampuni inafanya biashara bila
kulipa kodi anapaswa kutoa taarifa TRA au kwa Mkuu wa TAKUKURU Mkoani
Manyara kwa namba za simu 0738150124 kwa manufaa ya Taifa.
Amesema
endapo suala hilo likijitokeza ni bora taarifa zitolewe na hatua
kuchukuliwa kama zilivyochukuliwa kwa kampuni ya Mati Super brands Ltd
kuliko kufanya kama Chambo alivyofanya na kuhukumiwa kwenda jela.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...