Bendi maarufu ya muzuki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band almaarufu kama FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani imemwaga pongezi kwa  serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais  Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa tena kwa kishindo kikuuu kuingoza Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano tena.

Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja alitoa pongezi hizo kwa niaba ya bendi yake alipokuwa akiongoe studio za media City ziliopo katika mji wa Amsterdam,Holland ambako alikuwa akifanya ziara fupi ya vyombo vya habari nchini Uholanzi.

Kamanda Ras Makunja amewapongeza wa Tanzania kwa kupiga kura kwa amani na kuonyesha mfano bora wa kuigwa  na nchi zingine za Kiafrika, akisema kwamba Tanzania imeionyeshea maajabu duniani  kwa kufanya uchaguzi kwa kutegemea za pesa zake za ndani.
Ras Makunja amewaomba Watanzania wanaoishi nyumbani na nje ya Tanzania kushiriki katika ujenzi wa Tanzania wa viwanda na uchumi,pia kuitunza amani ya Tanzania daima milele.
Bendi hiyo, inayoendelea  kutamba na CD ya "Awamu Ya Tano Uwanjani", imeingia jikoni kupika kibao kingine cha kumpongeza Rais Magufuli kwa ushindi wa gharika ambao. haujapata kutokea katika historia ya Tanzania.

SIKILIZA KIBAO CHAO CHA AWAMU YA TANO KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...