……………………………………………………………………………………..
MBUNGE wa Jimbo la
Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, amesema atahakikisha
anakula sahani moja na watumishi wa Halmashauri hiyo wasiotekeleza
ilani ya CCM na kutimiza ahadi zilizoahidiwa kwa wananchi.
Ole Sendeka ameyasema
hayo wakati akiwashukuru wananchi wa Kijiji cha Lerumo kata ya Ruvu
Remiti alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo na kuwashukuru kwa
kumchagua.
Amesema atashirikiana
kikamilifu na watendaji wote wa serikali kwa asilimia 100 wanaoamini
na kutii maelekezo ya Rais John Magufuli na ambao wenye nia njema ya
kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Amesema watumishi
wasioelekea kwenye kutekeleza ilani na ahadi walizoahidiwa wananchi
kutoka siku ya kwanza wajue atawasonga hadi dakika ya mwisho.
“Nataka niwaambieni
awamu hii ya tano kipindi cha pili ambacho mimi ni mbunge nitashirikiana
na watendaji wote wa serikali kwa asilimia 100 wanaoamini na kutii
maelezo ya Rais John Magufuli na ambao wanania njema ya kutekeleza ilani
ya uchaguzi ya CCM,” amesema Ole Sendeka.
Amesema watumishi wa
serikali ni marafiki zake na kuanzia siku alipoapishwa mpaka siku
atakapomaliza kipindi chake ila wale ambao hawataelekea kwenye
kutekeleza ilani na kutekeleza ahadi walizoahidi wananchi kutoka siku ya
kwanza watambue atawasonga hadi mpaka dakika ya mwisho.
Amesema anaamini
madiwani waliopita siyo wala rushwa na wamepata Mwenyekiti wa
halmashauri makini Baraka Kanunga na Makamu wake Sendeu Laizer
wawajibikaji katika kusukuma vyema gurudumu la maendeleo ya wana
Simanjiro.
“Kazi iliyobaki ni
madiwani kwenda kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri, na nina amini
madiwani tulionao siyo wala rushwa hivyo watampa ushirikiano mwenyekiti
wa Halmashauri yetu,” amesema Sendeka.
Amewashukuru viongozi
wa dini kwa kuwaheshimisha kwa madhehebu yao yote kwa kuwaunga mkono
harakati za kuombea kupata uongozi hadi harakati za kushukuru, hivyo
wananchi wawaamini viongozi waliopo madarakani kwani watafanya na
kutekeleza yote waliyoyaahidi.
Amewashukuru viongozi
wastaafu wakiwemo madiwani na wenyeviti wa vijiji kwa kuwaachia alama
nzuri wakiongozwa na diwani mstaafu Peter Tendee na kwa wale ambao bado
wapo naye madarakani bado wanakibarua chakufanya katika kuwatumikia
wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...