Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Hassan Khatib
Hassan wakati alipowasili katika Soko la Wajasiriamali wadogo wadogo
Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo Changamoto mbali
mbali zinazowakabili .[Picha na Ikulu.] 18/11/2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi akiwapungia mkono Wafanyabiashara Ndogo Ndogo katika Soko la
Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara
ya Kikazi kujuwa changamoto mbali mbali kwa Wafanaybishara hao.[Picha na
Ikulu.] 18/11/2020.
Mkurugenzi wa Jiji la Zanzibar Ali Khamis Juma alipokuwa akimkaribisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi (katikati ) wakati alipotembelea soko la Kijangwani Wilaya ya
Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo kujua changamoto zinazowakabili
Wafanyabiashara ndogo ndogo sokoni hapo.[Picha na Ikulu.] 18/11/2020.
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo wakimsiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)
wakati alipozungumza nao na kuwataka kuwana subira wafanyiwe maamuzi
sahihi ya kupatiwa Eneo jengine la kufanyika Biashara zao kwa
uhakika,aliyasema hayo leo katika soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini
Mkoa wa Mjini Magharibi .[Picha na Ikulu.] 18/11/2020.
Mfanyabiashara Rashid Othman Matola akitoa maelezo kwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi
(hayupo pichani) wakati alipowatembelea leo wakiwa ma Mzozo wa kutakiwa
kuondoka katika Eneo hilo la Kijangwani na Uongozi wa Mkoa wa Mjini
Magharibi ambapo walipewa siku tatu.[Picha na Ikulu.] 18/11/2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wajasiriamali
wadogo wadogo katika Soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini
Magharibi leo alipofanya ziara ya kujuwa Changamoto mbali mbali
zinazowakabili wafanyabiashara hao.[Picha na Ikulu.] 18/11/2020.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...