Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema Ujenzi wa Stand mpya ya Mabasi ya mikoani ya Mbezi Luis umefikia 90%  na itaanza majaribio ya Kwanza November 25 na kuanza kutumika rasmi November 30.

Kutokana na hilo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye stand hiyo ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hotel ambapo zoezi la kutuma maombi limeanza leo November 09 Hadi November 25.

Aidha RC Kunenge amesema uwepo wa stand hiyo itaendelea kufungua fursa za maendeleo kwa Wakazi wa Ubungo hivyo amewataka kujiandaa kwa hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...