Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii

HIFADHI za taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika bara ya Afrika kwa mwaka 2020.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi- Mawasiliano, Pascal Sheltete, imesema tuzo hizo zimetangazwa jana Novemba 9, 2020 na taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya Mtandao.

ITaarifa hiyo imesema kuwa hii ni mara ya pili kwa hifadhi ya taifa ya Serengeti kushinda katika kundi la hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi bara la Afrika.

"Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za central kalahari  ya Botswana,  Etosha ya Namibia, Kidepo Valley ya  Uganda Kruge ya Afrika Kusini na Masai Mara National Reserve ya Kenya."

Imeeleza kuwa Serengeti inajivunia umaarufu wa Msafara wa Nyumbu uhamao zaidi ya milioni Moja na nusu,aina mbalimbali za wanyama pori wanaopatikana kwa wingi, maadhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimbali za utalii zinazovutia watalii wengi.

Aidha TANAPA imeishukuru serikali, wananchi, wadau wa utalii pamoja na watu wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya serengeti kuwa mshindi wa hifadhi boara zaidi kwa bara la Afrika 2020. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...