Na Amiri Kilagalilia,Njombe
Mbunge wa viti maalumu mkoani Njombe Neema Mgaya amekabidhi msaada wa taulo za kike 1600 zenye thamani ya shilingi milion 4 kwa wanafunzi wa kike katika za sekondari Maria Nyenyere,Makambako sekondari,Yakobi sekondari na Manyunyu sekondari. zitakazo weza kuwasaidia wanapokuwa hedhi.
Mara baada ya kukabidhi taulo hizo amesema, ametoa taulo hizo baada ya kutambua changamoto zinazowakabiliwa watoto wa kike pindi wanapokuwa hedhi.
Mbunge huyo amesema wanafunzi wengi hasa wa kike wamekuwa wakishindwa kusoma kwa bidii hasa wanapokuwa hedhi kutokana na kuathirika kisaikolojia kwa sababu ya kukosa vifaa hivyo.
Afisa elimu taaluma halmashauri ya mji wa njombe HURUMA CHAULA amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakifanyiwa matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kupata ujauzito hasa wanapokuwa katika kipindi hicho kutokana na kutopata elimu na vifaa husika.
Mkuu wa shule ya sekondari Yakobi iliyopo wilayani Njombe EDITHA HEDRICK JOHN amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao na kuwasaidia taulo hizo za kike ili waweze kushiriki vipindi vyote wakiwa shuleni.
Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari yakobi wamesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa baadhi ya vipindi shuleni hasa wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na kukosa taulo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...