Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UBALOZI wa Serikali ya Ufaransa nchini Tanzania umesma kuwa nchi yao imetenga Euro milioni 120 ambazo zitatumika kwa ajili ua mambo ya kijinsia kupitia katika mashirika na taasisiza kiraia ambapo pia wamezindua kampeni ya siku 16 kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Kwa mujibu wa ubalozi huo ni kwamba mpango huo ni wa miaka mitano katika kushughulikia masuala ya jinsia ulimwenguni kote na kwa Tanzania fedha hizo zitatumika kufadhili miradi miwili ya kuwawezesha wanawake kuzalisha asilimia 50 ya chakula na kuimarisha uwezo wa wanawake kwa kuwasaidia kupitia uwezeshaji wenye thamani ya Euro milioni 1.5 kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu mpango huo , Balozi wa Ufaransa nchini Fr'ed'eric Crevier amefafanua kwamba fedha hizo Euro milioni 120 zimetengwa na nchi yak kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kijinsia ulimwenguni.

Wakati akieleza hayo Balozi Clevier pia walikuwepo mabalozi na wawakilishi kutoka nchi nyingine wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na maofisa wengine kutoka Umoja wa Ulaya.Ajenda kuu ilikuwa ni kuzungumzia hatua za kuchukua katika kukabiliana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Balozi amesema kuwa kupigana na ukatili wa Kijinsia ni suala lenye kipaumbele kikubwa na linahitaji kuangaliwa kwa karibu kwa kushirikiana na serikali na Taasisi zingine zikiwepo asasi za kiraia na mashirika ya UN.

“Siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia ni kampeni muhimu za kumulika Ukatili wa Kijinsia na kufanya kazi pamoja ili kuleta mabadiliko ya tabia wakiwemo wanaume pia” amesisitiza.

Wakati huo huo Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti na mabalozi wengine wanachama wa Umoja huo ambao wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wakishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kwa pamoja wamezungumzia kuzinduliwa kwa Kampeni hiyo maalum ya siku 16 yenye lengo la kupinga ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake.

Kwa upande wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UN Women Tanzania Ms.Lianne Houben ameeleza kwamba katika siku 16 za kampeni za kupinga ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake zitaanza 25 hadi Desemba 10,2020 ambapo wameandaa shughuli mbalimbali zitakazofanyika ndani ya Dar es salaam.

"Pia kampeni hiyo itafanyika katika Mkoa wa Pwani ikiwa ni mkakati wa kuifikia jamii ya watu na kisha kupatiwa kile ambacho kimepangwa kutolewa wakati huu wa kampeni.Ujumbe muhimu wa Umoja wa Ulaya na inchi zingine wanachama.

"Kwa mwaka huu ni Maendeleo ya Mwanamke ni faida kwa Jamii Nzima ambayo imeunganishwa kwa karibu na kauli mbiu ya taifa la Tanzania ya 2020, inayosema Tupinge Ukatili wa Kijinsia. Mabadiliko yanaanza na Mimi," amesema Houben.

Aidha ameongeza lengo kuu la mwaka huu ni kukuza uelewa wa watoto kuhusu upungufu wa kuondoa Ukatili wa Kijinsia kupitia uwezeshaji wa wanawake kiuchumi huku maadhimisho ya mwaka huu yakiwa na washiriki kutoka katika Taasisi za kijamii (TACCI).

Pia Jukwaa la Heshima la Watoto (CDF) na watu mashuhuri kama vile Millad Ayo, Idris sultan, Dina Marios, Dkt.kumbuka na Dida Shaibu pamoja na Wasanii wa Uchoraji na wafanyabiashara wachanga wa kike pia wametajwa kushiriki.

Hata hivyo katika kukamilisha siku hizo 16 ujumbe wa Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Ufaransa, Ujerumani na Ubelgiji watafanya tukio la kuhamasisha umma chini ya kaulimbiu inayosema “Usiku wa Wanawake kuwezeshwa”

Huku lengo la hafla hiyo ni kutengeneza nafasi itakayomuwezesha mwanamke wa kitanzania kuweza kujieleza sambamba na maonyesho ya msanii wa kike pamoja na mawasilisho mafupi kutoka kwa wanawake wanaoanza.

Katika mkutano huo pia bazolo.ujeruman nchini Netherlan na wengineo walizungumzia tukio hilo muhimu la kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na kwa namna nchi zao zinavyoshiriki kikamilifu katika kulabiliana na changamoto hiyo hususani duniani.

Mkurugenzi wa Taasisi ya TACCI, Aline Uwamahoro akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Mkuu wa Ushirikiano Ubalozi wa Belgium, Jasmien De Winne akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsiaMkuu wa Ujumbe wa Jumuiya ya Ulaya, Manfredo Fanti akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Fredereck Clavier akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
Makilishi wa UN Women, Hodan Addou akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsiaBalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kuhusu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...