UKUAJI wa kasi wa miji nchini Tanzania kuna hitaji uelewa mazingira yanayosibu watoto katika miji hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya ESRF DktTausi Kida
wakati akitoa maneno ya ukaribisho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
kujadili na ukusanyaji wa maoni ya wadau mbalimbali kuhusu ukuajiwa miji
na athari zake kwa watoto.
Kwa
mujibu waDkt Kida kundi hilo la watoto na vijana ndio wanaotengeneza
hali ya badaae ya maendeleo yaTaifa. Moja ya tatu ya watanzania, kiasi
cha watu milioni 23, wanaoishi katika miji wapo chini ya miaka 18.
“
Vijana hao wanapoelekea utu uzima wanakumbana na matatizo mengi ya
kijamii na kiuchumi, matatizo ambayo kama yasipoangaliwa na kupatiwa
ufumbuzi yanadhuru maisha yao ya baadae” anasema Dkt. Kida.
Dkt.
Kida alisema katika hotuba yakekwamba kwa kuangalia miji ya Dar es
salaam na Mwanza unaona kwamba sirahisi kutambua changamoto na pia
fursa zilizopo kutokana na ukweli kuwa hakuna takwimu za kutosheleza
mahitaji ya uchambuzi wa mazingira yanayogusa watoto hao.
Anasema
kutokana na haja hiyo, kongamano hilo la kwanza limelenga kuleta pamoja
wadau wote kuzungumzia masuala hayo na kuyapatia muundo bora wa
ufumbuzi kwa lengo la kushauri watunga sera.
Pamoja
na kueleza nia ya mkutano Dkt. Kida pia alishukuru Mfuko wa Watoto wa
Umoja wa Mataifa(UNICEF) Tanzania kwa kuwa mshirika mzuri katika mradi
huo ambao upo ndani ya mradi wa Maabara ya Miji Tanzania (TULab) ambao
ESRF wametengeneza ramani ya utekelezaji wa maendeleo ndani ya miji.
Aidha alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango naTamisemi kwa kuwezesha kuwapo kwa tathmini ya watoto na vijana wa mijini.
TULab
ni sehemu katika mpango wa kuendeleza miji katika ilivyoainishwa katika
Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa 2016/17 – 2020/21
Kwa
mujibu wa Dkt. Kida,TULab inaendelea kusaidia juhudi za kitaifa za
utengenezaji wa sera na kutambua athari zinazokabili miji ya Tanzania.
Akifungua
mkutao huo Dkt. Mukuki Hante, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji kutoka
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alisema
kwamba Tulab ni jukwaa ambalo linasaidia serikali kuona maendeleo ya
miji na athari zake na namna ya kujipanga.
Alisema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa unajazia tatizo la watoto na fursa zao katika ukuaji wa miji.
Aliwataka wajumbe kutoa mawazo ili kusaidia utengenezaji mpango wa uchambuzi masuala ya watoto na vijana katika miji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya miji Wizara ya Tamisem, Dk Mukuki Hante akifungua mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akielezea mradi huo wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Dk Audax Kweyamba akizungumzia haki ya watoto ya kucheza na kushiriki maisha ya mijini wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Dk Rehema Mzimbiri akizungumzia masuala ya usalama wa chakula na lishe miongoni mwa watoto na vijana katika miji wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Bw. Joseph T. Baitwa (kushoto) akizungumzia masuala ya ulinzi kwa watoto na vijana dhidi ya ukatili wa kijinsia, kunyonywa na kususwa wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya miji Wizara ya Tamisem, Dk Mukuki Hante akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida.
Baadhi ya washiriki wakichangia maoni wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakichangia maoni wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki waliohudhuria mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...