Na Amiri Kilagalila,Njombe
Walimu
na Wasimamizi wa Mitihani Mkoani Njombe Wametakiwa kuacha kushiriki
Vitendo Vinavyo ashiria Utoaji wa Rushwa katika Kipindi Cha Mitihani ya
Kidato Cha nne na Chapili inayotarajiwa Kufanyika Siku za Usoni Hapa
nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na Ruswha (Takukuru) Mkoa wa Njombe Kassimu Efreim Wakati
Tasisi hiyo ikitoa Elimu kwa Club za Wapinga Rushwa Zilizoundwa Katika
Mashule mabalimbali Mkoani hapa Zenye Lengo la Kukemea Vitendo Vya
Rushwa.
"Tunaomba sana wasiamizi wa mitihani zingatieni sheria
kanauni na taratibu wa usimamizi wa mitihani ya serikali ,tunategemea
kusiwe na ushawishi wa rushwa na takukuru tupo"alisema Kassimu Efreim
Mwalimu
Sreven David Mwakila Kutoka Mpechi Sekondary Pamoja na Mwalimu Adbelta
Mgaya wanasema kuwa Wamekuwa Wakitoa Elimu kwa Wanafunzi juu ya Madhara
ya Rushwa huku Wakitaja Madhara Yenyewe na Namna yanavyoathiri Jamii.
"Tunaweza
tukapata wataalamu ambao hawajakizi vigezo lakini vile vile uchumi wa
taifa unaweza ukadidimia mfano zikajengwa barabara mbovu na mwisho wa
siku zikaharibika,kwa hiyo sisi kama walimu tumejifunza mengi na
tutawaambia wenzetu kwamba rushwa ina atahari kubwa sana kwa taifa letu"
Je?Wanafunzi Wenyewe Wanaelewa Nini Kuhusu Madhara Ya Rushwa katika Jamii na Hata katika Kipindi Cha Mitihani.
"Kwa
kweli tunapata elimu kuhusu madhara ya rushwa kwa njia mbali mbali kwa
mfano watu wa Takukuru kufika shuleni kwetu lakini pia matamasha mbali
mbali,na rushwa ina atahari nyingi mfano kupata wataalamu wasiokidhi
vigezo"walisema baadhi ya wanafunzi
Rushwa ni Adui wa
Haki,Serikali,Wadau mbalimbali Wamekuwa Wakikemea Vitendo Vya bRushwa
Ili Kuweka Usawa katika Jamii Baina ya Mwenye Nacho na Asie Nacho.
Kassimu Efreim Mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe akizungumza na wanafunzi
wa Club za Wapinga Rushwa Zilizoundwa Katika Mashule mabalimbali mjini
Njombe
Walimu wakiwa makini kusikiliza ofisa wa takukuru juu madhara ya Rushwa.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...