Katibu wa CCM
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ally Kidunda (kushoto) na Makamu
Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Albert Msole ambaye ni
Diwani mteule wa Kata ya Ngorika, Albert Msole.
……………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu, Manyara
Madiwani watano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamejitokeza kuwania
nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na madiwani wawili kuwania
umakamu Mwenyekiti.
Katibu wa CCM Wilaya
ya Simanjiro Ally Kidunda, amesema madiwani wateule saba wamejitokeza
kuwania nafasi hizo mbili kupitia CCM.
Kidunda amewataja
madiwani wateule hao waliochukua na kurejesha fomu ni Diwani wa kata ya
Ngorika na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha miaka minne
Albert Msole, Diwani wa Kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga (Mardadi) na
Diwani wa kata ya Komolo, Baraka Kanunga.
Amewataja waliochukua
fomu wengine ni Diwani mteule wa kata ya Langai na aliyekuwa Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Jackson Sipitieck na diwani mteule wa kata ya
Naisinyai, Taiko Laizer.
Amesema diwani mteule
wa kata ya Orkesumet Sendeu Laizer na kata ya Terrat Jackson Ole Materi
wamemchukua fomu ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa halmashauri.
“Zoezi lilakalofuata
ni wagombea hao kujadiliwa kwenye vikao vya kamati za siasa za wilaya na
mkoa ili kuchuja majina kwa ajili ya kuchaguliwa,” amesema Kidunda.
Diwani mteule wa Kata
ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Mardadi) akizungumza baada ya kuchukua
na kurudisha fomu ya kugombea amesema ana imani jina lake litarudishwa
na CCM na madiwani watamchagua.
“Nimekuwa na uzoefu
wa miaka mitano wa kuwa Diwani kwenye halmashauri yetu hivyo huu ni
wakati wa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Simanjiro,” amesema Mardadi.
Kwa upande wake,
Msole amesema uzoefu wa miaka minne wa nafasi ya umakamu Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo unatosha kumpa fursa ya kukamata nafasi hiyo.
“Pamoja na hayo elimu
niliyonayo nayo itachangia kuhakikisha naongoza kuitoa halmashauri yetu
hapa ilipo hadi kwenye maendeleo zaidi ya haya tuliyonayo,” amesema
Msole.
Sipitieck ambaye ni
diwani mteule wa kata ya Langai, amekiri kuchukua fomu ya kuomba
kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Diwani mteule wa kata
ya Naisinyai, Taiko Laizer amesema amejipima na kuona anatosha kuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Kanunga amesema
anaomba nafasi hiyo kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wa
Simanjiro na madiwani wake na kuwasemea mahali popote pale nchini.
Aliyekuwa Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo na Diwani mteule wa kata ya Orkesumet,
Sendeu Laizer amesema anaomba kuchaguliwa tena ili waendelee maendeleo
waliyoyafanya.
Diwani mteule wa kata
ya Terrat, Jackson Ole Materi amesema anaomba nafasi hiyo ili
kuwatumikia wananchi kwani anao uzoefu wa uongozi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...