IMEELEZWA kuwa kundi la Vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi umri wa miaka 24 ndilo kundi linalopata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kasi kubwa nchini.

Akiongea katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kimkoa yaliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square katibu Tawala Dodoma Keissy Maduka Amesema Takwimu zinaonyesha kuwa Asilimia 44 la kundi la Vijana lipo kwenye hali hatarishi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ukimwi.

Katibu Tawala huyo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema katika kipindi cha miaka ya 2012 hadi 2014  Mkoa wa Dodoma  ulikuwa ni miongoni mwa  mikoa yenye maambukizi madogo kwa asilimi 2.4.

 "Sasa tumeweza kuona takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaonyesha kuwa hali ibadilika ambapo kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2017 hali ya maambukizi mkoa wa Dodoma ni asilimia 5 hivyo Dodoma yetu imeweza kuingia kwenye mikoa hatarishi hakika hili ni tatizo kubwa hasa kwa Vijana wetu," Amesema Katibu Tawala Maduka.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika siku hiyo kujitokeza kwa wingi kwa kupima na kutambua afya zao mapema na kuacha uoga wa kujua afya zao kuwa kigezo cha kuhofia kufa Mapema.

" Kila mmoja wetu apime na atambue afya yake kwani ukipima na ukijitambua Mapema kama unamaambukizi ya virusi vya Ukimwi unanafasi ya kuishi vizuri kwa amani na furaha," amesema.

Kwa Upande wake mratibu wa Ukimwi mkoa wa Dodoma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Abdih Ahmed amesema visababishi vya Ukimwi havitofautiani na vingine katika bara la Afrika kuwa na wapenzi wengi, ngono zembe, kuchagua vitu vyenye ncha kali na hata ukatili wa kijinsia.

Amesema visababishi hivyo  vimechangia ongezeko kikubwa la Vijana kuwa na maambukizi na kuwa na idadi kubwa la watoto yatima .

"Takwimu kutoka NBS zinaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2017 Dodoma ilikuwa asilimia 5 ya maambukizi tofauti na mwaka 2013 mpaka 2014 ali ya maambukizi ilikuwa 2.9 hivyo Hali ya maambukizi Dodoma imeongezeka," amesema mratibu huyo. 

Akitoa ujumbe,mwakilishi kutoka  TACADS  Yeriko Kawanga amesema ukimwi bado ni tishio .

"Kwa mujibu wa takwimu zilizopo katika kila watu 100,watu wanne wana maambukizi, hili janga la Taifa." Amesema.

Amewataka wananchi waendelee kyjitojeza kupima Afya zao ili waanze kupatiwa tiba mapema.

Naye AnnaMary Osca akisoma risala ya Vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi amezitaja  changamoto mbalimbali zinazowakabili huku akiwataka vijana kujitokeza wekupima Afya zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...