Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akihubiri katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa
kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu
kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch.
Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa
nchini. 
Baadhi ya waumini wa Kanisa la
Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa
kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu
kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
la Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch.
Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa
nchini. 
Askofu Mkuu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch.
Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, mara
baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa
katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa
amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05,
2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini
wa kanisa hilo hapa nchini. 
Baadhi ya waumini wa Kanisa la
Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa
kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu
kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
la Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch.
Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa
nchini. 
Katibu Mkuu wa Kanisa la
Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania,
Mchungaji.David Makoye akiongoza maombi katika ibada ya kumshukuru Mungu
kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi
Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa
Kanisa la Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania,
Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(kushoto), iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa
hilo hapa nchini. 
Kwaya kutoka Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu
kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi
Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa
Kanisa la Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania,
Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa
la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo
hapa nchini.
Kwaya
kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Sabasaba Musoma mkoani Mara
ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika
Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani
hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista
Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin
Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista
Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
******************************************
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo ameongoza viongozi na mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona na Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini.
Ibada hiyo imefanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi mjini, Waumini wa kanisa hilo na wengine kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wamewawakilisha waumini wengine hapa nchini, ambapo ibada hiyo imehudhuriwa pia na viongozi wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
“Nilikuwa naangalia takwimu za hali ya janga la Corona ilivyo duniani leo asubuhi (yaani Desemba 05, 2020) hadi sasa zinaonesha watu 66, 281,000 wamepatwa na Corona, waliokufa mpaka sasa 1,525,294; ikiwa ulikuwa umechukulia kiurahisi, hizi takwimu zikuamshe kwamba Mungu ametupendelea sana Tanzania na tunamshukuru sana Mungu kwa niaba ya Watanzania wenzetu,” alisema Dkt. Lekundayo.
“Moja ya vitu ambavyo namshangaa Mungu ni kwa namna alivyotupendelea Watanzania maana na sisi ni wenye dhambi kama ilivyo kwa nchi zinazotuzunguka, sisi ni wenye dhambi kama ilivyo kwa mataifa mengine, lakini Mungu ametupendelea Tanzania na hivyo tunayo sababu ya kumshukuru Mungu maana amekuwa mwema sana kwetu” aliongeza Dkt. Lekundayo.
Awali akitoa mahubiri kabla ya maombi hayo pamoja na kuwasihi waumini kumshukuru Mungu kuwapitisha katika janga la Corona, Askofu Lekundayo pia ametoa wito kwa waumini kuendelea kumshukuru Mungu kwa namna ambavyo amelipitisha Taifa katika Uchaguzi Mkuu ambao umemalizika salama.
Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema Tanzania kupitishwa katika Janga la Corona haikuwa bahati bali ni neema ya Mungu, hivyo akawashukuru viongozi wa Dini kukubali wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuliombea Taifa kwa juhudi na Mungu akajibu na kulivusha Taifa letu.
Aidha, Kiswaga amesema Serikali inaheshimu mchango wa kanisa na itaendelea kushirikiana nalo katika majukumu yake ya kitume na kimaendeleo, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze kufanya kazi kwa manufaa na ustawi wa Watanzania.
“Katika neno la Mungu kuna habari ya wale wakoma kumi ambao waliponywa na Bwana Yesu lakini aliyerudi kushukuru ni mmoja tu, ninaamini maombi haya ya shukrani yataendelea kuiponya nchi yetu na majanga ambayo yanaonekana kwa macho na ambayo hayaonekani, ninawaomba viongozi wetu wa dini muendelee kuliombea Taifa, kumuombea Mhe. Rais na wasaidizi wake pia” alisema Kiswaga.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye amesema baadhi ya watu walimbeza Mhe Rais Magufuli alivyotangaza kumtanguliza Mungu wakati wa janga la Corona kwa kutangaza siku tatu za kuliombea Taifa, lakini anaamini kuwa baada ya kuona matokeo ya maombi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika, wameshuhudia kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi na kuahidi kuwa kanisa litaendelea kumuunga mkono Mhe. Rais.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...