Na ANNE ROBI - Mtwara
BARAZA la madiwani Jimbo la Tandahimba, Mkoani Mtwara limeazimia kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika jimbo hilo kwa kuweka mipango mizuri ya matumizi ya mapato yanayopatikana ndani ya halmashuri ya Tandahimba.
Wakizungumza mara baada ya kuapishwa na kufanya uchaguzi wa viongozi, Madiwani hao walisema wanayo mipango mingi ya kimaendeleo ambayo wamepanga kuitekeleza ndani ya miaka mitano ijayo kuleta mageuzi makubwa ya maendeleo.
Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmadi Katani alitaja baadhi ya mipango hiyo kuwa ni kufanya mabadiliko katika zao la korosho kwa kuwapa elimu wakulima na kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, kujenga barabara za ndani na kutekeleza mradi mkubwa maji Makonde.
“Katika mambo ambayo ni ya faraja kubwa ni mimi kuwa mbunge kwa kupitia chama cha CCM, chama ambacho kinashika dola, na kwa vyovyote iwavyo, miaka yangu hii mitano ni sawa na miaka 30 kwangu, kwa miaka hii mitano tutarajie tandahimba mpya, ambayo itakuwa ni ya kuingwa kwa mkoa wa Mtwara na ambayo itakuwa ni ya mfano kwa Tanzania,” amesema.
Katani ambaye anakwenda kutumikia jimbo hilo kwa miaka kumi ikiwa mitano ya mwanzo nyuma alitumikia wananchi akiwa chama cha upinzani, amesema chama chake mwanzo kilikuwa hakina Raisi wala baraza la mawaziri na kuja kwake CCM ataweza kuleta maendeleo kwa Tandahimba kwa uraisi sana.
Tunakwenda kufanya mabadiliko ya maendeleo kwa wilaya ya Tandahimba, mojawapo ya mabadiliko hayo itakuwa ni kwenye ukuaji wa zao la korosho,” alisema.
Ametaja mipango mingine ambayo baraza limepanga kutekeleza kuwa ni swala la barabara za ndani na mradi mkubwa wa Makonde ambao utasaidia kusambaza maji kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Madiwani Baisa Baisa amesema baraza hilo litashirikiana na halmashauri na wataalam wa kilimo kuweza kuwapa elimu wakulima, na kuwasaidia kupata pembejeo kwa wakati.
“Miongoni mwa vitu ambavyo vinasababusha uzalishaji wa korosho kuwa mdogo sa hivi ni ucheleweshwji wa upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, unakuta mkulima mpaka inafaki mda wa parizi, hana uwezo wa kupata pembejeo, “ amesema
Amesema atahakikisha wanashauriana na mafisa kilimo wa kata na viongozi wengine wa kata zote Tandahimba, na kuweka mikakati ambayo itasaidia ukuaji wa kasi na watija wa zao la korosho.
Akiongea katika hafla hiyo Mkurengezi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandhimba Said Msomoka amesema kwamba kuna matumaini makubwa kwa baraza hilo kuweza kuleta mageuzi makubwa ya maendeleo kwa jimbo la Tandahimba.
“Kutokana na hamasa ambayo nimeiona miongoni mwa madiwani, hali itakuwa ni nzuri kwa maana ya ushiriki wao kwenye kuchangia mawazo, ushauri, nina Imani kubwa sana na wao,” amesema
Amesema baraza hilo halitakuwa na malumbano ambayo hayana tija kwa kuwa sehemu kubwa ya madiwani ni wa upande mmoja na kuweka matumaini kwamba maendeleo yatakuwepo kwa sababu wataongea lugha moja
Jimbo la Tandahimba lina kata 32 na mbili ambapo kata 30 zinawakilishwa na madiwani wa upande wa CCM na kata moja kutoka chama cha ACT huku kata moja ikiwa haina diwani ambapo uchaguzi wake utafanyika hapo baadae.

Mwenyekiti wa baraza la Madiwani Tandahimba Baisa Baisa akizungumza Mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo.
Mwenyekiti wa baraza la Madiwani wa Jimbo la Tandahimba Baisa Baisa akizungumza katika haflya ya kula kiapo na kuchagua viongozi was madiwani wa Jimbo la Tandahimba


Baadhi ya madiwani wa Baraza la Madiwani Tandahimba wakia kiapo



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...