Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Innocent Bashugwa akizungumza na Watendaji wa Baraza la
Michezo la Taifa (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara katika Baraza
hilo pamoja na Naibu wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega (hayupo
pichani) ambapo ameahidi kuliimarisha Baraza hilo. Ziara hiyo imefanyika
Desemba 18,2020Jijini Da es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na Watendaji wa Baraza
la Michezo la Taifa (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara katika
Baraza hilo na Waziri wa wizara hiyo Mhe. Innocent Bashungwa (alievaa
shati ya maua) ambapo amelitaka baraza hilo kufanya mapinduzi katika
kuendeleza michezo. Ziara hiyo imefanyika Desemba 18,2020Jijini Da es
Salaam. Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashugwa na Naibu
wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega wakisikiliza na kufuatilia
uwasilishaji wa taarifa ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kutoka kwa
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bi.Neema Msita ambapo ameahidi
kuliimarisha Baraza hilo. Ziara hiyo imefanyika Desemba 18,2020Jijini Da
es Salaam.
************************************
Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa atahakikisha analiimarisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia na kuendeleza michezo nchini ikiwemo kuvisimamia vyema Vyama vya Michezo.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo Desemba 18, 2020 Jijini Dar es Salaaam wakati alipofanya ziara pamoja na Naibu wake Mhe. Abdallah Ulega katika Baraza hilo ambapo amesema Sheria zote ambazo zinahitaji kufanyiwa maboresho zitawasilishwa bungeni kwa ajili ya kufanyiwa maboresho yanayohitajika.
“BMT lazima msimamie ustawi wa timu zetu za Taifa, ni lazima turudi katika misingi ya Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA ambayo yanaibua vipaji vingi, nasisitiza timizeni wajibu wenu mliopewa kisheria bila kumuonea mtu”, alisema Mhe.Bashungwa.
Kwa upande wake Mhe. Naibu wa Waziri wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa BMT lazima ifanye mapinduzi katika kuendeleza michezo yote kwakua michezo inaleta ajira, inakuza uchumi na kuimarisha afya, huku akimuagiza Msajili wa Vyama vya Michezo kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa weledi na viwango katika kusimia vyama hivyo.
“BMT lazima mkae mguu sawa katika kutekeleza majuku yenu, ni jukumu lenu kuonyesha mafanikio kutokana na mafungu mbalimbali mnayopokea ya kuendesha michezo kwa uwazi na ukweli”, alisema Mhe.Ulega.
Mhe. Naibu Waziri Ulega ameongeza kuwa suala ya Tuzo kwa wanamichezo ni jambo jema ambalo linatakiwa kutekelezwa haraka ili kutambua mchango wa wanamichezo nchini.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph singo amesema kuwa sekta hiyo imepata mafaniko mengi ikiwemo timu za wanawake za mpira wa miguu kutwaa makombe mbalimbali Afrika, Timu ya vijana chini ya miaka 17 kushiriki AFCON 2019 yaliyofanyika hapa nchini na timu ya vijana chini ya miaka 20 kufuzu AFCON 2021.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bi. Neema Msita amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ya Baraza hilo ni kuboresha baadhi ya Kanuni ambazo zimeleta mafaniko ikiwemo kutambulika kwa michezo ya ridhaa na ya kulipwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...