MSANII wa muziki wa kizazi kipya Behnam Paul a.k.a Ben Pol ameachia video ya wimbo wake mpya Kidani ambao amemshirikisha mke wake Anerlisa kama video vixen.
Wimbo huo umeachiwa siku ya jana, 9 Desemba 2020 chini ya mtayarishaji Hanscana.
Ben Pol amesema video hiyo imefanyika ndani ya Jiji la Dar es Salaam na imetoka katikati ya sintofahamu ya ndoa ya wawili hao baada ya kusemekana kuwa imevunjika.
"Video hii inaweza kuwa ni uthibitisho kuwa ndoa yangu nna Anerlisa bado iko imara, na. pia naendelea kutoa shukrani za dhati kwa wapenzi wangu kwa ushirikiano wanaonipa na nimeona niandae burudani kwao"amesema Ben Pol.
Amesema kuwa ameandaa usiku maalum utakaofanyika Desemba 31 utakaofanyika Ramada Hotel ili kutoa burudani kwa mashabiki wake.
Ben Pol amesema kuwa siku hiyo atashusha burudani ya kufungia mwaka na amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ili kuanza mwaka kwa pamoja.
Hivi karibuni kulikua na taarifa ya kuvunjika kwa Ndoa ya Ben Pol na mkewe Anerlisa na sintofahamu hiyo ilizidi kushika kasi baada ya msanii huyo kubadili dini na kuingia katika Uislamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...