TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, imeadhimisha siku ya maadili kwa kusikiliza kero za wananchi
Vijijini.
Mkuu wa
TAKUKURU Wilayani Simanjiro, Adam Kilongozi ametoa elimu ya rushwa na
kusikiliza kero za wananchi kwenye Kijiji cha Oiborkishu Kata ya Oljoro
namba tano.
Kilongozi amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na dhuluma bila kutishwa na mtu yeyote.
Amesema hivi karibuni wananchi wa eneo hilo walitoa malalamiko yao TAKUKURU kwamba wanachangishwa michango bila kupewa risiti.
Mmoja
kati ya wananchi wa eneo hilo Robert Mollel ameipongeza TAKUKURU kwa
kufuatilia suala hilo kwani wananchi walikuwa wanachangishwa michango
bila kupewa risiti.
Amesema
baada ya kutoa taarifa TAKUKURU juu ya kitendo hicho hatua za haraka
zimechukuliwa hivyo wananchi kuwa na imani na serikali yao.
Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Adam Kilongozi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Oirboikishu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...