Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Dkt.
Charles Mwamwaja, akimkabidhi Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB,
Fredrick Nshekanabo, tuzo ya mshindi wa kwanza kwa upande wa taasisi za
fedha ya uwasilishaji bora wa hesabu kwa mwaka 2018/2019 kwa kutumia
viwango vya kimataifa vya kutayarisha hesabu zilizotolewa na NBAA
===== ===== =====
BENKI
ya CRDB imeibuka kinara katika tuzo zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya
Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kama taasisi ya fedha iliyoongoza
kwa kuwasilisha Taarifa ya Fedha bora kwa mwaka 2018/2019 kwa kuzingatia
viwango vya kimataifa.
Akikabidhi
tuzo hiyo, Dkt. Mwamwaja ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea
kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa katika utayarishaji wa
taarifa zake za kifedha. Dkt. Mwamaja alisema kuandaa ripoti za mwaka za
Mashirika na Taasisi za Umma kwa viwango vya kimataifa kunawapatia
wananchi fursa ya kupima ufanisi wa utendaji kazi wa taasisi husika,
kuona namna gani yanawajibika ipasavyo katika kutumia rasilimali.
“Hongereni
sana Benki ya CRDB kwa kuibuka kinara katika upande wa taasisi za
fedha, hii inadhirisha ni jinsi gani Benki hii imewekeza katika mifumo
ya kisasa ya kutoa huduma kwa wateja lakini pia na kuwezesha kupata
taarifa za kiwango,” alisema Dkt. Mwamwaja.
Akizungumzia
ushindi huo, Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nsekanabo,
amesema Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa kuandaa taarifa za fedha
kupitia mifumo inayozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa. Alisema
kitendo cha kupata tuzo hiyo kunaifanya benki hiyo kuendelea kuongeza
jitihada ili kubaki katika nafasi hiyo.
“Tumefanya
uwekezaji mkubwa katika mifumo ya kidijitali hii ni pamoja na kuboresha
mifumo yetu ya kukusanya na kuandaa taarifa. Tumeweza pia kuunganisha
mfumo wetu wa utoaji taarifa za fedha na mfumo wa kimataifa wa kuandaa
taarifa za fedha (IFRS), hii pia imechangia Benki yetu kuwa bora zaidi,”
alisema Nshekanabo.
Nshekanabo
alibainisha kuwa ushindi huo pia unatokana na Benki hiyo kuwa wa mfumo
bora wa uongozi unaozingatia weledi, uwazi wa taarifa za kifedha,
uwajibikaji na kiwango cha juu cha uadilifu wa takwimu.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mr.Pius Maneno, alisema Benki ya CRDB
imeibuka kinara baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na taasisi
hiyo kwa zaidi ya asilimia 75. Kwa mwaka 2019 taasisi 61
zimeshindanishwa katika tuzo hizo za NBA zilizo jumuisha vipengele 13.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...