RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 8/12/2020.(Picha na Ikulu)

………………………………………..

Makamo wa kwanza wa Rais mteule Maalim Seif Sharif Hamad aliyeapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk Hussein Ali Mwinyi ametakiwa kufanya kazi kwa dhati na kukiheshimu kiti cha Rais.

Ikiwa  kiongozi huyo ameingia kwenye suk kwa lengo la  kushindana na Rais ili aje kumtoa madarakani katika Uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025 maelewano tarajiwa yatapwaya.
Ushauri huo umetolewa  Balozi Mstaafu Ali Abeid Karume  mara  baada ya Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kumuapisha  huko ikulu na kuwa rasmi Makamo  wake wa kwanza wa Rais.
Balozi Karume amesema licha ya  Maalim Seif ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu, anapaswa kukiheshimu kiti cha Rais kwani Dk Mwinyi ndiye mwenye urais.
Ameitaja kazi ya Maalim Seif kwa mujibu wa katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 ni kumshauri Rais na kutekeleza majukumu yote  atakayopangiwa na Rais.
Balozi Karume amesema  ukongwe wa Maalim Seif katika medani za siasa na utawala kisiwe kigezo cha kumfanya adhani yuko sawa na Rais au Rais atapokea maelekezo kutoka kwake.
Amesema  badala yake kazi alionayo  ni ya ushauri kwa Rais hivyo Rais atakuwa na hiari ya kukubali ushauri huo au kuukataa.
Aidha Balozi amsema ikiwa kiongozi huyo wa upinzani kwa dhati yake aheshimu matakwa ya Rais kisera, kimalengo na kimajukumu  anaamini kazi ya kujenga nchi itafanyika kwa umakini.
Mtoto huyo wa pili wa Rais wa Kwanza  Zanzibar hayati Mzee Abeid Amanj Karume ,amesema kila mwanasiasa ajue  urais haupatikani kwa njama au kwa mizengwe.
Badala yake amesema urais  humfika yeyote  kwa  kudra, bahati na uweza wa mungu wala si kwa  hujuma au kwa makeke.
Mwadiplomasia huyo amekitaja chanzo cha mvutano katika  suk awamu ya saba amedai kulikuwa na hali ya kutoelewana kati ya Rais na Makamo wake wa kwanza wa Rais.
Amesema jambo la kusikitisha baadhi ya siri za SMZ zikizagaa mitaani kabla hata ya vikao vya BLM havijamalizika Ikulu.
Amemtaja Maalim  Seif kuwa ndiye aliyeanza  kumtupia vijembe Rais kwenye mikutano ya hadhara ,  Rais   alipoona mambo yanazidi akamjibu na hapo  ndio ufa ulipojitokeza.
Amesema hadi wanakwenda katika Uchaguzi mwaka 2015 maelewano yao yalishatetereka hivyo akasema hategemei kama hali hiyo itajirudia tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...