Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akimsikiliza mmoja wa Mameneja wa Mgodi wa North Mara Hilaire Diarra akitoa maelezo kuhusu uhifadhi wa tope sumu (TFS), mwenye shati la Kijani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, kushoto kwa waziri Mkurugenzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Dkt. Mwanga, na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Mwita Waitara.

Waziri wa Madini, Doto Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila wakiteta jambo wakati wa ziara yao mgodi wa North Mara.

Waziri wa Madini, Katikati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila mwenye koti jeusi, Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima mwenye shati la Kijani na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wakiwa wanaagana baada ya kumaliza ziara.

Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akimsikiliza Mkurugenzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Dkt. Mwanga akitoa maelezo kwa Waziri kuhusu uhifadhi wa tope sumu (TFS), kulia kwa Dkt. Mwanga ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Mwita Waitara.

****************************************

Na, Issa Mtuwa, Mara

Imeelezwa kwamba mgodi wa North Mara umekiuka Sheria ya Ushirikishwaji wa Watanzania (locol content) baada ya kutangaza zabuni nje ya nchi na kupata mzabuni kinyume  cha sheria za Madini.

Hayo yamesemwa tarehe 18 Desemba, 2020 na Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kufanya ziara maalum mgodini hapo.

Kanuni za Madini (Ushirikishaji wa Watanzania), 2018 Tangazo la Serikali Na. 2/2018 zinataka wamiliki wa migodi kutangaza zabuni hapahapa nchini na endapo hakuna mtanzania mwenyewe sifa au vinginevyo, zabuni hiyo inatangazwa nje ya nchi na atakaepatikana atalazimika kushirikiana na Mtanzania. Biteko amesema, kwa mujibu wa sheria hiyo, mgodi utakaokiuka utatozwa adhabu ya dola za kimarekani milioni tano. Ameongeza kuwa sheria hiyo inalenga kutoa fursa ya watanzania katika kushiri masuala ya uchumi wa madini.

Country Manager, wa Mgodi wa North Mara, Hilaire Diarra, alikiri kosa kutofuata sheria kwa kuwa walikuwa katika presha ya kutekeleza mradi huo. Diarra ameomba radhi na kwamba wapo teyari kufuata maelekezo yatakayo tolewa na Serikali.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeo ya jamii (CSR), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alihoji kuhusu utekelezaji wa (CSR). Meneja Mgodi anaeshughulikia Mahusino Gilbert alisema wametekeleza kwa kujenga madarasa, kujenga visima vya maji na masuala ya afya japo Prof. Msanjila alimwambia hawajafuata utaratibu unao takiwa katika kutekeleza miradi ya CSR.

Kutokana na majibu hayo, Biteko ameuagiza mgodi kuanda mpango wa utekelezaji wa miradi ya CSR na kuwasilisha kwenye mamlaka ya serikali za mitaa ili waipitie na kuidhinishwa teyari kwa ajili ya kutekeleza. Akizungumzia kuhusu masuala ya fidia, Biteko amesema wanaolipwa ni wale wenye haki akisisitiza kuwa utaratibu wa mtindo wa watu ku tegesha hawawezi kulipwa fidia.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amesema suala la fidia nyamongo linacheleweshwa na wananchi kutokwa na mchezo wa suala ya tegesha. Amesema watu watakao bainika sheria itachukuwa mkondo wake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...