*Boomplay watoa takwimu za muziki 2020
APP namba
moja kwa huduma ya muziki Barani Afrika, Boomplay imemtaja msanii Rayvanny kuwa
ndiyo mwanamuziki wa kiume aliyesikilizwa zaidi Tanzania huku Zuchu akiwa ndiyo
mwanamuziki wa kike aliyesikilizwa zaidi Tanzania. Hii ni kwa mujibu wa taarifa
na takwimu rasmi za muziki kwa mwaka 2020.
Taarifa
hiyo iliyowekwa kwenye ripoti maalumu kuhusu muziki imeegemea zaidi kwenye data
kutoka katika app hiyo ya muziki ambayo kwa mwezi ina wastani wa watumiaji
milioni 50 ulimwenguni kote. Boomplay inajivunia kuwa na aina tofauti za nyimbo
ambazo idadi yake ni zaidi ya milioni 44, ambazo zinapatikana kwenye iOS,
Android na web huku ikiwa na jumla ya wasanii milioni 3.4 duniani kote.
Kwa kuanza
na wasanii wa kiume watatu wa kwanza waliosikilizwa zaidi nchini Tanzania, Rayvanny
anashika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Diamond Platnumz katika nafasi ya pili
huku Harmonize akishika nafasi ya tatu.
Wasanii wa
kike watatu wa kwanza nchini Tanzania waliosikilizwa zaidi ni Zuchu akishika
nafasi ya kwanza akifuatiwa na Nandy katika nafasi ya pili huku Maua Sama
akishika nafasi ya tatu. Zuchu pia ametawala katika kipengele cha Nyimbo tatu
kutoka kwa wasanii wa Tanzania zilizoongoza kusikilizwa ambazo ni Wana, Raha na
Kwaru, zote hizo kutoka kwenye albamu ya Zuchu ‘I am Zuchu’.
Burna Boy ameongoza orodha ya wasanii wa kiume waliosikilizwa zaidi katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara huku Simi akifanya hivyo kwa upande wa wasanii wa kike.
Boomplay pia imetoa taarifa za mwenendo na tabia za namna muziki unavyosikilizwa Tanzania. Katika taarifa hiyo maalumu, Bongo Flava imeongoza kwa kusikilizwa ikifuatiwa na nyimbo za Injili (Gospel) huku Afropop & Afrofusion ikishika namba tatu.
Zaidi, angalia hapo chini orodha kamili ya Boomplay 2020 Music Facts Tanzania. Msanii wako umpendaye, wimbo au albamu umeona? Tuambie!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...