Kufuatia
uwepo wa Changamoto mbali zinazohusu Umeme Maeneo mengi hapa Nchini,
Naibu Waziri wa Nishati Adv. Stephen Byabato (Mb) ametoa mwelekeo wa
Wizara husika katika kutafutia Ufumbuzi Kero sugu za Umeme
zinazowakabili Wananchi ambao kipekee ndio Watumiaji wa Nishati hiyo.
Naibu
Waziri Byabato ambaye yupo Mkoani Kagera kwa Ziara ya Kikazi,
ameoneshwa kusikitishwa na Kero ndogo ndogo zinazoendelea kuwakumba
Wateja na Watumiaji wa Umeme, ambazo Ni Ukosefu wa Mita, Nyaya, Nguzo na
wakati mwingine Uzembe, sababu ambazo zimeainishwa na Wananchi kutoka
Maeneo mbalimbali Mkoani Kagera wakati wakitoa Kero zao, katika Ukumbi
wa Mkuu wa Mkoa Kagera Desemba 22, 2020.
Miradi
yote ya Umeme inayotekelezwa Nchini, hasa maeneo ya Visiwani na sehemu
ambazo Umeme haujawafikia Wananchi, kuhakikisha Shirika la Umeme hapa
Nchini TANESCO kuhakikisha wanasimamia Gharama za uuzaji wa Umeme huo
kwa Wananchi, kulingana na Maelekezo Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani Juu ya punguzo la Umeme huo, kwani maeneo mengine wamekuwa
wakiuziwa Umeme zaidi ya Shilingi 100 kwa Unit moja.
Katika
suala la wale ambao wameomba kuunganishiwa Umeme na bado
hawajaunganishiwa kwa sababu mbalimbali na kupelekea suala Hilo kuchukua
Muda Mrefu, Mhe. Byabato ameagiza TANESCO kutumia muda wa Siku Saba tu
kukamilisha Mchakato wa Upembuzi na Tathimini ikiwa ni pamoja na Vipimo,
kuanzia siku mteja akiomba Huduma hiyo, Kisha baada ya hapo Mteja
akalipie gharama ya uunganishwaji Umeme kwa Shilingi 27,000/= Ndani ya
Siku Tisini, na kuongeza kuwa wale wote ambao wameomba kuunganishiwa
Huduma hiyo Ndani ya Mkoa Kagera wawe wameunganishiwa Huduma ya Umeme
kufikia Tarehe 31 Januari 2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...