*********************************
Mkoa wa Dar es salaam
Leo umetoa taarifa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha
Kwanza kwa mwaka 2021 ambapo jumla ya watahiniwa 76,430 sawa na 86.94%
wamefaulu mtihani huo na kufanya Mkoa huo kuongoza kitaifa.
Akitoa taarifa ya
wanafunzi waliochaguliwa, Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.
Paul Makanza amesema jumla ya wanafunzi 61,504 waliofaulu wamepangiwa
kujiunga na kidato Cha Kwanza awamu ya Kwanza na wanafunzi 14,926
waliofaulu watapangiwa shule awamu ya pili.
Aidha Bw. Makanza
amesema jumla ya vyumba 299 vinahitajika kujengwa ili kupokea wanafunzi
hao ambapo Hadi Sasa vyumba 350 vinaendelea kujengwa Katika Manispaa
mbalimbali na vinatarajiwa kukamilika kabla ya February 28 mwaka 2021.
Hata hivyo Makanza
amewataka wazazi na walezi kuwapeleka wao kwenye shule walizopangiwa
ifikapo January 11 mwakani bila kukosa na kuwataka Wakuu wa shule
kuwapokea wanafunzi bila kikwazo chochote hususani michango.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...