Na Amiri Kilagalila,Njombe

MKUU wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni ameelekeza viongozi wa wilaya hiyo na kata ya Igima Kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukusanyaji wa Michango ya ujenzi wa bweni Jipya la wavulana katika Shule ya sekondari Igima lililoungua Moto Mwezi Septemba mwaka huu na kuteketeza Kila Kilichokuwamo Ndani pasina Kuleta Madhara Kwa Wanafunzi Wenyewe.

Ametoa agizo hilo wakati akipokea mifuko 250 ya Saruji Toka Shirika la Nyumba La Taifa NHC Kwa ajili ya Kuanza Ujenzi wa Bweni Hilo na Kwamba Makubaliano ya Mchango wa Shilingi Elfu Kumi Kila Mwananchi Yatekelezwe Haraka Kabla Hatua za Kisheria Hazijaanzachukuliwa.

“Naelekeza mtendaji wa kijiji,kata na bodi ya shule vile viwango ambavyo kila mwananchi inatakiwa achangie lazima achangie basi achangie na ikipendeza kabla ya tarehe 25 jengo liwe limesimama na vimebakia vitu vidogo vidogo”alisema Lauteri Kanoni

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Edec Lukoa amesema kutokana na changamoto ya kupanda kwa saruji Katika kipindi kilichopita kiliwalazimu kusimamisha ujenzi wa bweni Hilo Lakini Kwa  Wanaendelea na Hadi kukamilika linatarajiwa kutumia zaidi ya Shilingi Milioni 75 fedha ambazo Ni michango ya Serikali,Wananchi Pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo.

“Hilo bweni liliungua lote kabisa na watoto kama 90 walitoka salama wenzetu shirika la nyumba walipokea ombi letu na waliahidi kutusaidia kama tulivyoomba”alisema  Lukoa

Said Bungara Ni Meneja wa Shirika la Nyumba NHC mikoa ya Njombe,Iringa na Mbeya ambaye anasema wao Kama Wadau baada ya kupewa taarifa ya kuungua kwa Bweni Hilo waliona Ni muhimu kuchangia Nusu ya mifuko ya saruji  ili wanafunzi waendelee kuishi Katika mazingira salama.

“Shirika la nyumba ni wadau wa maendeleo na tunaunga mkono jitihada za serikali yetu na tuliposkia kuna jambo la kuchangia kwa watoto wetu tukasema na sisi tujitoe vile ambavyo tunaweza na tukatoka mifuko 250 ambayo ni sawa na tani 12.5”alisema Said Bungara

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igima Mika Mbembati na Judy Kinyamagoha Wamesema Hatua Zinazoendelea Kuchukuliwa na Serikali Katika Ujenzi wa Bweni Hilo Zinawapa Matumaini ya Usalama wa Maisha Yao Pamoja na Masomo Huku mkuu wa shule hiyo Edwin Sanga Akishukuru kwa msaada huo na kuwaomba Wadau mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono Kwa Kuwa Bado Kuna Uhitaji Mkubwa wa Mabweni.Baadhi ya wananchi wa kata ya Igima waliofika kwenye mapokezi ya saruji wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe.

Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe akizungumza na wananchi waliofika katika mapokezi ya mifuko hiyo ya saruji kutoka shirika la nyumba la taifa.
Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe akipokea mifuko ya saruji kutoka kwa meneja wa shirika la Nyumba la taifa NHC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...