Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

DIWANI wa Viti maalumu CCM Kibaha Mjini, Mh.Lidya Mgaya, amekarabati nyumba za kukandika udongo za wazee zipatazo saba, huko Kongowe na kusema wazee ni hazina ya Taifa hivyo yatupasa kuwasaidia pale inapobidi.

Diwani wa Viti maalumu CCM Kibaha Mjini, Lidya Mgaya, ameamua kuanzisha oparesheni yake aliyoita *Lidya Kazini* kuwafikia wananchi na kuwagusa katika maisha yao kwa kufanya ukarabati wa nyumba zao za udongo kwa kuzikandika na kurejesha fito na minengo katika nyumba ambazo zimeharibika na nyingine kubomoka.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la ukandikaji wa nyumba saba wazee na waasisi wa CCM, Diwani Lidya alisema muitikio wa Oparesheni ya Lidya Kazini umekuwa mkubwa tofauti na alivyotarajia wakati akipanga na mratibu wake kuhudumia nyumba hizo.

"Kwanza namshukuru mratibu wa Oparesheni Lidya Kazini, Komredi Jumanne Kambi kwa kufanikisha jambo hili vijana ni wengi wamejitokeza kila tawi kushiriki pamoja nami kurejesha furaha kwa familia za wazee wetu tumekandika na kuzikarabati kwa kiasi chake nyumba hizo;

"Kwa jinsi nilivyoona hili zoezi kwa jinsi nitakavyojaliwa kipato litakuwa ni zoezi endelevu kwa maana nyumba ni nyingi za wazee wetu zenye shida mbalimbali zenye kuhitaji msaada kutoka kwetu sisi viongozi na watu wengine wenye mioyo ya kujitoa", alisema Diwani Lidya.

Wakiongea kwa nyakati tofauti Mzee Seif Nzowa wa Mtaa wa Kongowe na Mzee Anthony Thomas wa Mtaa wa Mwambisi ambao ni baadhi ya wazee na waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao nyumba zao zimeguswa na zoezi hilo walimpongeza diwani Lidya kwa uamuzi aliofanya juu ya kuwakarabatia nyumba zao.

" Kiongozi bora huonekana kwa kugusa na kuyaishi maisha ya wananchi wa hali ya chini kwa jinsi atakavyoweza kujaliwa kusaidia kulingana na kipato cha mfuko wake alichonacho."walisema

Naye mratibu wa shughuli hiyo, Komredi Jumanne Kambi, aliwapongeza wanachama wa ccm na jumuiya zote kwa ujumla waliojitokeza kumsapoti Diwani Lidya katika kufanikisha zoezi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...