Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kustukiza usiku wa manane kwenye Ujenzi wa Soko la Tandale kwa lengo la kujionea Kama maagizo aliyotoa yametekelezwa.

Miongoni mwa maagizo aliyotoa RC Kunenge kwenye Ziara aliyofanya Jumamos ya Disemba 19 ni pamoja na kumtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na Mchana na kuongeza idadi ya vibarua na kweli amekuta Mkandarasi huyo ametekeleza angizo kwa kufunga taa na anafanya kazi ya kumwaga Zege ambapo amemuelekeza kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika kabla ya mwezi wa nne mwakani Tena kwa ubora unaotakiwa.

Aidha RC Kunenge ametuma Salamu kwa wakandarasi wote wanaotekeleza miradi Jijini humo kuzingatia mikataba yao kwa kuhakikisha wanakamilisha miradi kwa wakati ili iweze kutatua kero za wananchi Kama Serikali ilivyokusudia.

 Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...