Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson leo amepewa kuwa mama mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Jerusalem kinachosimamiwa na kanisa la KKKT Kimara.
Akizungumza
katika ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Kimara
jijini Dar es Salaam, Mchungaji Kiongozi, Wilbrod Mastai amesema kuwa
mbali na Mheshimiwa Dkt Tulia kuwa mlezi wa kituo hicho wameamua kumpa
kuwa mzazi wa hao watoto.
"Tumeamua
kumpa heshima ya pekee ya kuwa mzazi wa watoto 21 wa kituo chetu cha
kulelea watoto Yatima kinachosimamiwa na kanisa letu, hivyo tunamshukuru
kwa kuweza kukubali ombi letu," amesema.
Katika
tukio lililovuta hisia za waumini ni kubatizwa kwa mtoto mmoja kati ya
hao 21 Meshack Elinaza ambaye anawiki mbili tokea amepokelewa kituoni
hapo.
Kwa
upande wa Dkt Tulia Ackson ameshukuru uongozi wa kanisa la Kiinjili la
Kirutheri Tanzania (KKKT) Kimara kwa kuweza kumpa heshima ya kuwa mama
wa watoto hao, huku akiahidi kuwalea katika maadili ya kidini na kuweza
kumjua Mungu.
"Niwashukuru
kwa kunipa heshima ya pekee kwasasa nitakuwa nanyi bega kwa bega katika
kuwalea watoto hawa waliopo kituo chenu, sina mengi zaidi kuzidi
kushukuru na mzidi kuniombea ili niweze kuwa mama bora," amesema Dkt
Tulia Ackson.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...